Mjumbe wa Mkutano CCM Taifa kutokea Wilaya ya Temeke Mohamed Ally Mmanga alipojitokeza na kuchukua fomu ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Lumumba leo jijini Dar es salaam.
Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye amerudisha fomu ambayo alichukua Juzi ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Lumumba leo jijini Dar es salaam.
………………………
NA MUSSA KHALID
Mjumbe wa Mkutano CCM Taifa kutokea Wilaya ya Temeke Mohamed Ally Mmanga amejitokeza na kuchukua fomu ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza nimzoefu na anauwezo mkubwa katika uongozi.
Mmanga ambaye pia aligombea Ubunge jimbo la Mbagala Dar es salaam mwaka 2020 ameeleza hayo leo wakati akichukua fomu ya kuwania Uspika wa Bunge katika ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Lumumba jijini Dar es salaam.
Aidha Mmanga amesema kuwa anao uwezo mkubwa yeye kama Kijana ya kuwa Spika wa Bunge hivyo malengo yake atahakikisha anafanya kazi kwa vitendo na siyo kuwa na maneno maneno.
‘Mimi kama kijana ninauwezo sifa ninazo shule ipo hakuna tatizo lolote nina uwezo wa kusimama Bungeni kusimamia mazuri ya Bunge lakini pia kusimama na Mwenyekiti wangu wa chama Cha Mapinduzi Taifa Mama yetu Samia Suluh Hassan hivyo mutarajie mambo mazuzi kama Chama change kitapendelea na kunipa ridhaa hii ya kwenda kukiwakilisha bungni’amesema Mmanga
Mmanga ameendelea kusema kwa mujibu wa Katiba inamruhusu kila raia wa Watanzania kugombea nafasi ya Uspika hivyo atakapopata ridhaa atakwenda kufanya mazuri.
Wakati huo huo Aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Goodluck Ole Medeye amerudisha fomu ambayo alichukua Juzi ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema anasubiri vikao vya Chama viweze kuamua.
‘Namshukuru Mungu kwa idasi ya watu waliojitokeza inaonyesha Dmokrasia katika Chama chetu imekomaa kwamba kila mtu anafursa sawa na mwenzake kwa hivyo naupongeza Uongozi wa Chama kwa kuweka misingi hii inayotuwezesha kushikamana’amesema Ole Medeye
Ikumbukwe mpaka sasa wamejitokeza wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 30 ambayo wamechukua fomu ya kuwania Nafasi ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania