Mohammed Mmanga ambaye ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi na Mjumbe wa Kamati Kuu Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za CCM Lumumba
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Mohammed Mmanga(Kushoto) akichukua fomu ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Januari 13,2022.
………………………………..
KADA wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) wameendelea kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo binti wa miaka 32 anayefahamika kwa jina la Ester Stephano Makazi anayeishi Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Hadi jana Januari 12,2022 jumla ya waliokuwa wamechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo walikuwa 30 na leo Januari 13 mwaka huu wameendelea kuchukua kwa ajili ya kuomba ridhaa ndani ya CCM kupitishwa na hatimaye kupigiwa kura na wabunge.
Mohammed Mmanga, ambaye amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo Leo amesema amejitokeza kuwania nafasi hiyo kwa kuwa ana uzoefu wa muda mrefu kwani ameanzia chipukizi na ameendelea kukua akiwa ndani ya Chama.
Mmanga amesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa Spika atatumia kila aina ya maarifa aliyonayo kuhakikisha anasimamia maslahi ya Chama, Serikali na Taifa kwa ujumla
Mmanga ameongeza kuwa mejitathmini na kujiona anatosha kuchukua nafasi hiyo na endapo vikao vya chama chake vikimpitisha na kumteua kuwa mgombea basi bunge na taifa litegemee makubwa kutoka kwake kwani uwezo,nia nguvu la kulihudumia bunge analo.
Kabla ya kuchukua fomu hiyo Mmanga ambae kwa Sasa ni mjumbe mkutano mkuu taifa aligombea pia ubunge Jimbo la mbagala.