Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelice Mafumiko akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kikao cha wadau wanaohusika na usafirishaji wa Kemikali hatarishi leo jijini Dar es salaam.
Albert Swai kutoka kampuni ya CMTL Logistic ambao wanahusika na usafirishaji wa kemikali akiwaeleza waandishi wa habari namna wanavyofanya shughuli zao za usafirishaji wa kemikali.
…………………….
NA MUSSA KHALID
Wasafirishaji wa Kemikali nchini Tanzania wametakiwa kufata muongozo wa usafirishaji kutoka kwa Mkemia Mkuu kuhusu kuwa na vifaa vya kujikingia ili waweze kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza wawapo safarini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt Fidelice Mafumiko wakati akifungua kikao cha wadau wanaohusika na usafirishaji wa Kemikali hatarishi wakiwemo wawakilishi wa serikali TRA,LATRA,Mamlaka ya Bandari Pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa.
Dkt Mafumiko amesema kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanawakumbushana wasafirishaji hao sheria inayohusika na udhibiti wa kemikali zikiwemo hatarishi pamoja na kanuni zake.
‘Lengo kuu la udhibiti au usimamizi wa kemikali hizi hatarishi ni kulinda Afya ya wananchi pamoja na mazingira ya viumbe wote hai unakuta kwamba uingizaji wa kemikali hizi kwa sasa hivi imeanza kuja kwa wingi hivyo tunachofanya ni kuwafundisha wasafirishaji ili wafahamu nini wanapaswa kukifanya wanapokuwa wanasafirisha kmikali hatarishi’amsema Dkt Mafumiko
Aidha Dkt Mafumiko amewataka kuwa na utaratibu wa kutoa taarifa kwa wakati pindi wanakumbana na matatizo wakati wa usafirishaji wa kemikali hizo kwenye maeneo ambazo wanapita.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania COO-TAT Husein Wandwi amesema wamekuwa na changamoto ya baadhi ya maderva kutokuwa na elimu ya namna ya kujikinga na aina ya kemikali wanayoisafirisha.
‘Tunaona hii kwetu nii fursa kubwa sana sisi kama wasafirishaji kwa sababu mwongozo ukija utataka madereva wote waendeshule au wale wote wanaohusika katika kusafirisha kemikali wawe na elimu’amesema Wandwi.
Naye Albert Swai kutoka kampuni ya CMTL Logistic wakihusika na usafirishaji wa kemikali amesema serikali imekuwa ikiwaonyesha ushirikiano kwa kuwaongezea uelewa wa kielimu ili kuhakikisha kuwa madhara hayatokei.
Hata hivyo serikali imesema itaendelea kuwajengengea uwezo madereva hao wanaosafirisha kemikali ili waweze kukabiliana na madhara yanayosababishwa na kemikali hizo.