TIMU ya Namungo FC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Meli 4 City katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabao ya Namungo yamefungwa na Ali Saleh aliyefunga dakika ya 21 na Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 80 kwa penalti, wakati la Meli 4 City limefungwa na Hussein Mwinyi dakika ya 90