Muwakilishi Jimbo la Magomen,i ambae pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Jamali Kassim Ali akizungumza na Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni , katika Hafla ya Uzinduzi wa Huduma za Afya kwa ajili ya Wazee katika Jimbo hilo .
Muwakilishi Jimbo la Magomeni ambae pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Jamali Kassim Ali, akipimwa Presha katika Hafla ya Uzinduzi wa Huduma za Afya, kwa ajili ya Wazee katika Jimbo hilo .
Baadhi ya Wazee kutoka Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar , wakiwa katika Hafla ya Uzinduzi wa Huduma za Afya kwa ajili ya Wazee katika Jimbo hilo .
Mbunge wa Jimbo la Magomeni Mwanahamisi Kassim Said, akizungumza na Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Mjini Zanzibar, katika Hafla ya Uzinduzi wa Huduma za Afya kwa ajili ya Wazee katika Jimbo hilo .
PICHA NA MARYAM KIDIKO/ MAELEZO ZANZIBAR.
***************************
Na Kijakazi Abdalla Maelezo 2/01/2022
MWAKILISHI wa Jimbo la Magomeni ambae pia ni Waziri wa Nchi,Afisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali amesema wataandaa utaratibu wa kuwapatia bima ya afya wazee wa Jimbo la Magomeni.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa huduma za upimaji afya kwa Baraza la Wazee huko katika Skuli ya Maandalizi Magomeni amesema atashirikiana na viongozi ili kuwapatiwa bima ya afya ya wazee wa jimbo hilo.
Aidha amesema imebainika kuwa wazee wamekuwa anakabiliwa na maradhi mengi hivyo watahakikisha wazee wa jimbo hilo wanapatiwa huduma za afya zilizo bora.
Akizungumzia suala la maradhi ya UVIKO 19 Mheshimiwa Jamali amesema kuwa takwimu na tafiti zimeonesha kwamba maradhi hayo pale yanapowakumba wazee yamekua yakiwaathiri kwa kiasi kikubwa sana.
Aidha amewataka wazee hao kupata chanjo ya uviko 19 na kuondokana na maneno ya upoteshaji ambayo yamekuwa yakirejesha nuyuma juhudi za serikali.
“chanjo hii ni salama kwa afya zetu viongozi wetu wan chi tayati tumeshachanja na nitakuonesheni kadi yangu ili na nyinyi mwende mkachanje “Mheshimiwa Jamali aliwasisitiza Wazee wa Jimbo hilo.
Kwa upande wake Mjumbe kutoka Juwaza Ghania Othmani amewataka viongozi wa Jimbo la Magomeni kuwapa kipa umbele wazee wa jimbo hilo katika kuwapatia huduma bora za afya.
Amesema wazee ndio hazina ya nchi hii ambao waliyapigania Mapinduzi ya Zanzibar na hivi sasa tumekuwa tukitembea kifua mbele.
Nae Mbunge wa Jimbo la Magomeni Mwanakhamis Kassim Said amewahakikishia Baraza la Wazee wa jimbo hilo kuzitatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuwapatiw ofisi wazee hao pamoja na kuwapatia eimu ya wajasriamali.
Aidha amewataka wananchi ambao wanaishi na wazee kujenga utamaduni wa kuwapima afya wazee mara kwa mara ili kuondokana na maradhi.
Akisoma risala ya Baraza Wazee jimbo la Magomeni Maryam Haji Sheha amesema baraza hilo limekuwa na utaratibu wa kuwapima afya wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea bila ya kujali dini, jinsia na itikadi ya kisiasa.
Kwa upande Mratibu Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Fahad Mussa Mohd amesema lengo la zoezi la kupima afya kwa Baraza la Wazee wa Jimbo la Magomeni ni kuiunga Serikali katika kuazimisha miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapima afya kwani imebainika kuwa wazee wanakabiliwa na changamoto nyingi za maradhi mbalimbali.
Aidha amesema kwa upande wa vijana wameandaa utaratibu wa kuwapima virusi vya ukimwi pamoja na uvikio 19 kutokana na kuonekana kuwa vijana wengi wanaonekana kuwa wana njia ya viashiria hatarishi.
Nae bwana Simai Haji Mohd kutoka sogea amewashukuru viongozi wa Jimbo hilo kwa kuandaa utaratibu wa kuwapima afya wazee wa jimbo hilo na kuwaomba liwe endelevu.