MUANDAAJI wa Matamasha ya Pasaka na Christmas, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo uliofanyika ofisini kwake Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
MUANDAAJI wa Matamasha ya Pasaka na Christmas, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo uliofanyika ofisini kwake Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam leo kulia ni mdau wa masuala ya habari Bw. John Bukuku.
………………………………………
MUANDAAJI wa Matamasha ya Pasaka na Christmas, Alex Msama, ameungana na watanzania kumshukuru Mungu kwa kuwajalia kumaliza mwaka salama japo tumepitia mengi magumu na mazuri.
Amewataka watanzania kuanza mwaka mpya kwa kuendelea kumuunga mkono Mama Samia kwa makubwa anayoyafanya na kusema mikopo nikwaajili ya maendeleo ya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo jijini Dar es Salaam, Msama amesema watanzania waendelee kumuunga mkono Rais Samia kwa maendeleo anayoyafanya.
“Tunaimani na Rais wetu Samia japo ndie Rais wetu wa kwanza mwanamke lakini anaupiga mwingi kwenye kuleta maendeleo ya nchi yetu Tanzania.
“Pamoja na tuliopitia yote kufiwa na Rais Marehemu John Pombe Magufuli lakini Mungu ameendelea kulipigania Taifa letu na kumpa ujasiri Rais wetu.
Aidha ameongeza kuwa kuhusu mikopo kila nchi zilizoendelea zinajiendesha kwa mikopo hivyo Rais Samia mikopo anafanyia maendeleo ya Taifa nasio kujinufaisha na familia yake hii mikopo ni faida ya kila mwananchi kwa sababu inaenda kufanya maendeleo kwa ajili ya watanzania wote.