Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mchungaji Dkt. Barnabas Weston Mtokambali akizungumza kwenye kanisa la CITY CHRISTIAN CENTER (TAG) Upanga na kufanya maombi wakati waombolezaji mbalimbali waliposhiriki ibada ya Kuaga mwili wa aliyekuwa Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la TAG na Mchungaji Kiongozi wa kanisa la City Christian Center (TAG) Upanga Marehemu Askofu Ranwell Mwenisongole aliyefariki hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Ibada ya Kumuaga Marehemu Mwenisongole imefanyika leo Katika Kanisa la CITY CHRISTIAN CENTER (TAG) lililopo Upanga mkabala na Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam,Baada ya kuagwa Mwili wa Marehemu umesafirishwa kuelekea nyumbani kwao Kijiji cha Ichenjezya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe kwa Mazishi.
(PICHA NA JOHN BUKUKU)
“BWANA ALITOA BWANA AMETWA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE”
Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mchungaji Dkt. Barnabas Weston Mtokambali akiombea mwili wa Marehemu Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la TAG,Ranwell Mwenisongole wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza kwa niaba ya Serikali alipotoa salamu zake katika ibada hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Ranwell Mwenisongole.
Mtoto wa Marehemu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi George Mwenisongole akizungumza katika ibada hiyo wakati akitoa historia ya marehemu baba yake.
Picha mbalimbali zikionesha waombolezaji wakianga mwili wa Marehemu Askofu Ranwell Mwenisongole katika ibada iliyofanyika kwenye kanisa la CITY CHRISTIAN CENTER (TAG) Upanga jijini Dar es Salaam.