Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan L. Bukumbi akiambatana na Mkuu wa Usalama Barabarani wamefanya Operesheni katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa hususani eneo la Kitonga lakini pia kutoa elimu kwa Madereva ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika hasa kipindi hiki cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.
ACP Bukumbi amewakumbusha madereva kutii sheria za barabarani ili kuepuka ajali na kwamba hatosita kumchukulia hatua dereva yeyote atakaekiuka maadili ya udereva awapo barabarani.
Hali kadhalika Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Iringa, SP Yusuf Kamota ametumia muda huo kuwakumbusha kuwa Iringa sio sehemu sahihi kwa madereva wasiofuata sheria za barabarani na kwamba atahakikisha sheria zinatekelezwa ipasavyo.
Katika hatua nyingine, Kamanda Bukumbi amewataka abiria wawapo safarini, kutoa taarifa kwa wakuu wa usalama barabarani endapo kuna vitendo vya uvunjifu wa sheria kwani Jeshi la Polisi limeweka utaratibu wa kubandika mawasiliano kwenye Vyombo hivyo.