Ndugu William Erio Mkurugenzi Mkuu wa FCC akifungua rasmi semina ya wahariri wa habari za biashara kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania ambayo ilifanyika jana kwenye kituo cha mikutano cha Julius Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.
Dr. Allan Mlulla ambaye ni Mkurugenzi wa Miungano ya Makampuni, Utafiti na Uraghibishi FCC akitoa mada katika semina ya wahariri wa habari za biashara kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania ambayo ilifanyika jana kwenye kituo cha mikutano cha Julius Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.
Martha Kisyombe Mkurugenzi Utekelezaji wa Sheria FCC akifafanua mambo mbalimbali katika semina ya wahariri wa habari za biashara kutoka vyombo mbalimbali nchini Tanzania ambayo ilifanyika jana kwenye kituo cha mikutano cha Julius Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.
Magdalena Utouh Mkuu wa Idara ya Ukaguzi wa Bidhaa Bandia FCC akionesha moja ya bidhaa ambazo taasisi hiyo ina wajibu wa kuzilinda wakati wa semina ya wahariri wa habari za biashara kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini ambayo ilifanyika jana kwenye kituo cha mikutano cha Julius Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.,
Nsajigwa Wilfred Afisa Mawasiliano na Uhusiano Mkuu FCC akitoa utaratibu wa namna semina hiyo itakavyoendeshwa wakati akisoma ratiba.
Baadhi ya Picha zikionesha wahariri mbalimbali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika jana kwenye kituo cha mikutano cha Julius Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.
TUME ya Ushindani Tanzania(FCC), imesema wametoa siku 21 kwa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwasilisha taarifa muhimu za mkataba wa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, GSM na tayari shirikisho hilo limeanza kupeleka nyaraka hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 20, 2021 na Mkurugenzi wa FCC, William Erio wakati akifungua semina ya Wahariri wa Habari za Biashara iliyoandaliwa na tume hiyo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Suala la mkataba wa GSM linashughulikiwa sitaki kulizungumzia sana kwa sasa kwa sababu tumewapa TFF siku 21 kuleta taarifa muhimu na tayari zimeanza kuja,” amesema Erio.
Aeleza sababu ya FCC kuwanoa wahariri
Amesema lengo la FCC kuwapa semina wahariri wa habari za biashara ni kutaka kuwawezesha kuelimisha umma ambao ni walaji wa bidhaa ili wawe salama kwa kuepuka bidhaa bandia na wafanyabiashara wafuate sheria na watu wapya wanavutiwa kuwekeza Tanzania.
Kwa upande wake Katibu wa Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)Neville Meena, ameishukuru FCC kwa semina hiyo na kuwataka kuendelea kutoa nafasi hiyo kwa wanahabari ili wananchi waweze kuifahamu vizuri na shughuli zake.
“Nina ombi kwa ajili ya wanahabari wa ‘sports’, baada ya kundi hili kufikiria kukutana na waandishi wa sports kwa kuwa sasa hivi kuna uwekezaji mwingi wa kibiashara katika michezo,” amesema.
Yaeleza ukubwa wa tatizo la bidhaa bandia
Akitoa mada katika semina hiyo, Mkuu wa Idara ya Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Bidhaa Bandia, Magdalena Utouch, amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na vitu bandia hasa kutokana na ukuaji wa teknolojia.
Magdalena ameeleza kuwa changamoto hiyo inachangiwa na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kukosekana kwa ofisi za Kanda ambapo wanatarajia kuzifungua.
“Maana ya bidhaa bandia (feki)ni bidhaa zilizotengenezwa kwa kuiga bidhaa nyingine kwa nia ya kudanganya mlaji na mara nyingi huwa bidhaa duni na zina madhara makubwa kwa mlaji,” amefafanua kuhusu Majukumu ya FCC amesema
Kati ya majukumu ya FCC ni kuhakikisha hakuna makubaliano ya makampuni yaliyo kinyume cha FCA, kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria kwa makampuni au mtu anayetumia vibaya nguvu ya soko.
“Kwa kutambua umuhimu na nafasi yenu katika vyombo vya habari kama wahariri na waandishi waandamizi wa habari za biashara,sisi FCC ndiyo shughuli yetu kubwa hiyo. Tumeona ni vema kuwajengea uwezo na kuwaongezea uelewa wenu, tunafikiri baada ya kumaliza tutakuwa tumefanikiwa,”
“Kimsingi shughuli zetu ni mbili, kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara hapa nchini. Kuhakikisha kila kinachofanywa hakikiuki sheria ya ushindani, pia tuna jukumu kubwa la kumlinda mlaji,” amefafanua Erio.