Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene,akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kinachojadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2021 kwa mwaka wa fedha 2021/22, kilichofanyika leo Desemba 17,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene,akisisitiza jambo kwa washiriki wa Kikao cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kinachojadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2021 kwa mwaka wa fedha 2021/22, kilichofanyika leo Desemba 17,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Khamis Hamza Chilo,akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kinachojadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2021 kwa mwaka wa fedha 2021/22, kilichofanyika leo Desemba 17,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi na Katibu Mkuu – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu, Christopher Kadio,akitoa taarifa ya kikao hicho kilichofanyika leo Desemba 17,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (hayupo pichani) akifungua Kikao cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kinachojadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2021 kwa mwaka wa fedha 2021/22, kilichofanyika leo Desemba 17,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa huduma za uangalizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Aloyce Musika,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki mara baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kufungua Kikao cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kinachojadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2021 kwa mwaka wa fedha 2021/22, kilichofanyika leo Desemba 17,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kikao cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa wizara hiyo kinachojadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2021 kwa mwaka wa fedha 2021/22, kilichofanyika leo Desemba 17,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………….
Na Alex Sonna, Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amelitaka Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kujadili mambo yatakayosaidia kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya watumishi huku akiagiza Viongozi wa Wizara hiyo kuandaa ripoti ya wastaafu ambao hawajapata stahiki zao.
Simbachawene ameyasema hayo leo Desemba 17,2021 wakati akifungua kikao cha baraza hilo kinachojadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2021 kwa mwaka wa fedha 2021/22, kilichofanyika jijini Dodoma.
Amesema kuna wastaafu ambao wamekuwa wamekaa miaka mitatu bila kulipwa stahiki zao.
“Wajibu wa mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi ni kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao, pia wanazingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo ya utendaji wa kazi wenye tija, ufanisi, weledi, umahiri, staha na upendo,”amesema.
Aidha, ametaka kutumia kikao hicho kutoa mapendekezo na ushauri kwa wizara ili kutimiza malengo yake.
Pamoja na hayo, amewahimiza watumishi kuchanja chanjo ya UVIKO-19 na kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo.
Naye, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Khamis Hamza Chilo, amehimiza kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, amesema pamoja na uwapo wa mafanikio mbalimbali lakini bado kuna changamoto ya ukomo wa bajeti, uhaba wa watumishi na vitendea kazi.