……………………………………………….
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia SAIMON ASEGELILE KABETA [23], mkazi wa Kijiji cha Lema kwa tuhuma za kumjeruhi mguuni kwa kumpiga jiwe OMARY ASAGWILE KABETA [43] mkazi wa Kijiji cha Lema.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 16.12.2021 majira ya saa 02:00 usiku huko Kijiji cha Lema, Kata ya Busale, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya ambapo mtuhumiwa alimjeruhi kwa kupigwa jiwe kwenye mguu wake wa kulia na kusababishiwa jeraha kubwa lililopelekea kuvuja damu nyingi. Chanzo ni ugomvi uliozuka kati yao wakiwa wanakunywa pombe klabuni. Majeruhi amekimbizwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
KUKAMATWA MTUHUMIWA WA MATUKIO YA KUVUNJA NYUMBA MCHANA NA KUIBA.
Mnamo tarehe 16.12.2021 majira ya saa 04:00 asubuhi huko maeneo ya Uyole na Gombe, Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Askari Polisi wakiwa msako walimkamata MISSA NDELA [43] mkazi wa Uyole ambaye anatuhumiwa kwa matukio ya wizi na Kuvunja nyumba mchana na kuiba.
Matukio hayo ameyafanya maeneo ya Ilomba kati ya tarehe 13/12/2021 na 15/12/2021 kwa kuiba vitu mbalimbali. Upekuzi umefanyika na kukutwa na:-
- Mabegi mawili ambayo ndani yake kulikuwa na mali za wizi,
- Simu mbili aina ya Samsung Smart Phone,
- Ipad moja Apple,
- Nyaraka mbalimbali za ofisi,
- Vitambulisho mbalimbali,
- Diary mbili,
- Charger ya Laptop,
- Charger 03 za simu,
- Bluetooth moja,
- Picha za Passport size za watu mbalimbali.
KUFANYA BIASHARA YA MADINI BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 16.12.2021 majira ya saa 04:00 asubuhi huko Kijiji na Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi kwa kushirikiana na Maafisa Madini Wilaya ya Chunya wakiwa Misako waliwakamata 1. MICHAEL ZUMBA [33] mchimbaji madini, mkazi wa Matundasi 2. SAMSON JOHN [20] mkazi wa Matundasi 3. ADAM JOHN [40] Mkazi wa Matundasi na 4. YOHANA MAHENGA [24] mkazi wa Matundasi kwa kosa la kufanya biashara ya madini bila kuwa na kibali wakiwa na Gramu 3.5 za madini ya Dhahabu wakinunulia nyumbani.
KUFANYA BIASHARA YA MADINI BILA KIBALI.
Mnamo tarehe 16.12.2021 majira ya saa 06:30 mchana huko Kijiji na Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi kwa kushirikiana na Maafisa Madini Wilaya ya Chunya wakiwa Misako walimkamata ZAINABU CHARLES [30] mchimbaji madini, mkazi wa Matundasi akiwa na Gramu 20 za madini ya Dhahabu akinunulia nyumbani kwake bila kuwa na kibali.
Imetolewa na;
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.