Mkuu wa Mkoa Kigoma Mh Thobias Andengenye akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Murubona wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Mkuu wa Mkoa Kigoma Mh Thobias Andengenye akwa katika = uzinduzi wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Murubona wilayani Kasulu mkoani Kigoma kulia ni Mkuu wa wilaya Mh. Kanali Isack Mwakisu.
Baadhi ya madawati yakiwa yamepangwa katika moja ya madarasa yaliyokamilika kwenye shele ya sekondari ya Murubona wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Muonekano wa moja ya madarasa yaliyojengwa katika shule ya sekondari ya Murubona wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
……………………………………..
Mkuu wa wilaya Mh. Kanali Isack Mwakisu, ameongoza viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya mji wa Kasulu, kukabidhi Vyumba vya Madarasa 57 vilivyokamilika kwa asilimia 100% kwa Mkuu wa Mkoa Kigoma Mh. Thobias Andengenye,
Katika Hafla hiyo fupi iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya Murubona, mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Madarasa Mawili kupitia fedha za UVIKO 19 ambayo yamejengwa ndani ya Muda uliopangwa (15 Desemba, 2021).Shule ya Murubona inawakilisha Shule zingine za Mji wa Kasulu ambazo zimepitiwa na mradi huo.
Mkuu wa Mkoa amepongeza sana ushirikiano wa watendaji wa Kasulu mji kwa kuwa na Kasi yenye ufanisi Mkubwa katika Kukamilisha Mradi huo kwa wakati na ubora Mkubwa.
Amesisitiza kuwa ushirikiano huo uendelee ili kuleta Maendeleo Makubwa ya Mji wa Kasulu, yanayoweza kuleta Neema ya Mji huo kuwa Manispaa hapo Baadae.
Mradi wa Ujenzi wa madarasa 57 katika shule 17 wilayani Kasulu
Umegharimu shilingi za kitanzania bilioni 1 na milioni 140.
na umekamilika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliokuwa umepangwa kwa utekelezaji.