Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri.na kuibuka kidedea katika mashindano hayo.(Happy Lazaro)
………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Baadhi ya wanafunzi wa mchepuo wa sayansi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya wasichana Arusha wamefanikiwa kugundua kifaa cha matumizi ya viuatilifu kitakachowasaidia wakulima kutumia kuuwa wadudu mashambani pasipo kuathiri afya udongo,walaji pamoja na mkulima.
Wanafunzi hao wamesema wamebuni kifaa hicho kutokana na kuingia katika mashindano ya bunifu mbalimbali katika shule tano zilizopo mkoani Arusha ambapo walifanya tafiti kupitia wataalamu mbalimbali ambapo wakabaini changamoto ya wakulima katika matumizi ya sahihi viuatilifu.
“Kifaa hiki tumekigundua ambapo tunatumia harufu kuwavuta wadudu kuingia kwenye ndani ya kifaa na kukuta mafuta ya mmea wa mwarobaini kwa ajili ya kuwaangamiza kwani njia hii itamsaidia mkulima kulinda afya yake pamoja na mtumiaji wa mazao hayo,”amesema Nice Namanya
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa chuo cha ufundi Arusha,Mussa Chacha amesema kati ya eneo walioshindwa kwa miaka mingi ni elimu ya sayansi kuiunganisha na biashara ni vyema wanafunzi hao wakatilia mkazo katika eneo hilo la kuwa wabunifu katika kuvumbua vitu vitakavyosaidia jamii.
Josephine Sepeku ni meneja mradi kutoka chuo cha ufundi atamizi amesema lengo ni kuwasaidia wanafunzi ambao walikuwa wanapatiwa sayansi ya vitendo kuilinganisha pamoja na biashara ili kutatua changamoto katika jamii pamoja na kujiingizia kipato.
“Shule zilizoingia kwenye mashindano ya bunifu hizo ni pamoja na Arusha Sekondari,ilboru ,Edimund Rice,Bishop duning na Arusha girls,”amesema Sepeku.
Mmoja wa walimu Exaudy Mollela amewaomba wadau kujitokeza katika kuwekeza katika mawazo ya bunifu hizo ili kupanua wigo wa matumizi ya kifaa hicho kwani hawana vyanzo vya kutosha vya mapato
Kifaa hicho kinaitwa kifaa cha S -Vebla ambacho hutumia mafuta ya mmea wa mwarobaini kuvuta wadudu wanaokimbilia kwenye mazao badala yake kuingia kwenye kifaa hicho na kuangamizwa.