Bw. George Lugata Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania akionesha kwa waandishi wa Habari Simu mpya ya Samsung Galaxy A02 ambayo mteja ataipata kwa kianzio cha c shilingi elfu 80.000 tu katika maduka yote ya Kanda ya Vodacom kwa ushirikiano na kampuni ya d-light kushoto ni Charles Natai Mkurigenzi Mtendaji wa , d.light Tanzania mkutano huo umefanyika kwenye duka la Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurigenzi Mtendaji wa , d.light Tanzania akionesha Simu mpya ya Samsung Galaxy A02 ambayo mteja ataipata kwa kianzio cha c shilingi elfu 80.000 tu katika maduka yote ya Kanda ya Vodacom kulia ni Bw. George Lugata Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania
Charles Natai Mkurigenzi Mtendaji wa , d.light Tanzania akizungumza katika mkutano hio ambao umefanyika kwenye duka la Vodacom Tanzania Mlimani City jijini Dar es Salaam.
…………………………………….
Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwaletea wateja wake huduma na bidhaa zenye tija na manufaa zaidi.
Hayo yamesemwa na George Lugata Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania wakati akizindua huduma ya manunuzi ya simujanja kwa mkopo ambayo Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na D. Light imeleta kwa wateja wake.
Lugata amesema kupitia ushirikiano huu, mteja wa Vodacom atatakiwa kulipia Tsh 80,000 tu na ataondoka na simu yake, halafu atakuwa akilipia shilingi 1,800 kwa siku kwa muda wa siku 300 ili kumaliza deni analodaiwa.
Mpango huu ni Kukuza ujumuishwaji wa kidijitali tunataka kuhakikisha kila Mtanzania anapata simujanja na kama kampuni tumeandaa mikakati tofauti ili kufanikisha ongezeko la matumizi ya simujanja nchini, hii ni pamoja na kusambaza simu za bei rahisi kama smartkitochi ambayo inauzwa kwa TZS 38,000.
Lengo letu kuu ni kuwapa Watanzania wengi zaidi fursa ya kumiliki simujanja ili waweze kufaidika na huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia mfumo wa kidijitali nchini Tanzania.