Na Silvia Mchuruza
Bukoba,Kagera.
Zao la kahawa aina ya Robusta lmetajwa kuongeza tija na uzalishaji mkoani Kagera kupitia kwa wakulima wadogo wadogo licha ya kuwepo changamoto mbalimbali hasa changamoto ya kifedha
Kauli hiyo imetolewa na afisa biashara wa mkoa wa Kagera Ndg. Issaya Tendega aliekuwa mgeni rasmi katika kikao kilichowahusisha wadau wa zao la kahawa kupitia mradi wa Cafe Africa kilichofanyika katika ukumbi wa ELCT HOTEL BUKOBA kwa niaba ya katibu tawala ma mkoa.
Tendega amesema Licha ya kuongezeka kwa uzalishaji wenye tija kubwa katika zao la kahawa bado changamoto zipo hasa katika suala la kifedha na masoko.
Nae mkurugenzi wa Cafe Africa Bi. Dafrosa Sanga. amesema kuwa kahawa aina ya Robusta imeongezeka katika uzalishaji licha ya kuwepo vitendo vya Butura na mikahawa ya zamani kuwa mizee tayari ambapo mradi huu umefanya jitihada za kuchipusha tena mikahawa hiyo.
Aidha amesema kuwa Cafe Africa ni mradi wenye lengo la kuinua zao la kahawa kuliongezea thamani na tija kwa wakulima katika uzalishaji ambapo mradi huo ulikuwa na lengo la kuwafikia wakulima wa wilaya zote za mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na vyama vikuu vya ushirika KCU na KDCU.
Hata hivyo ameongeza kuwa vyama vya msingi vikubwa na vidogo vilivyolengwa kufikiwa ni 250 na wakulima 22250 ambapo pia mradi umetoa mafunzo kwa maafisa ugani 445, mpaka Sasa wamefikiwa wakulima 16384 na maafisa ugani 320 na kufanikiwa kuanzisha mashamba darasa 207.
Pia Bi. Dafrosa ameongeza kwa kusema mradi umeendelea kuboresha miundombinu kwa kushirikiana na wadau wa zao la kahawa ambapo tayari mradi umechipusha miti laki sita (600,000) na kukarabati vitaru 4 katika wilaya 4 kikiwemo kitaru Cha Maruku ili kuwainua wakulima katika uchumi wao kufikia mwaka 2025.