Pichani ni ujenzi wa jumba itakapo simikwa mitambo tisa ya kufua umeme (Power house) kwenye mradi wa Julius Nyerere.
Muonekano wa daraja la kudumu katika mradi wa Julius Nyerere.
:Eneo la kupokelea umeme (switch yard) linayoendelea kujengwa kwenye mradi wa Julius Nyerere.
…………………………..
Mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa megawati 2115 wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika bila ongezeko la gharama za ujenzi. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba Desemba 7, 2021 alipotembelea eneo la mradi akiambatana na Waziri wa Nyumba Maendeleo ya Makazi na huduma wa Jamuhuri ya kiarabu ya Misri Mhe .Assem Hafez El azar.
Ziara hiyo ilikuwa ya pamoja kati ya Nchi za Tanzania na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ambayo imepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi ya mwezi Novemba 2021, inayoonesha kuwa utekelezaji wa mradi unakwenda vizuri.
‘‘kwa dhamira na malengo ya mradi, na gharama zilizotumika, Serikali ya Tanzania haiwezi kuruhusu mradi huu kutokukamilika, kwa wenzetu wa Misri pia mradi huu ni chachu ya ushirika yenye manufaa kwao pia nao wako tayari kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa faida ya nchi zote mbili. ‘’ amesema Waziri Makamba.
Ameelekeza timu ya wataalam toka Wizara ya Nishati pamoja na TANESCO kuangalia changamoto zilizojitokeza na kuzifanyia kazi ili kuhakikisha mradi unakamilika kama Mhe. Rais Samia Suluhu Hasan alivyowaahidi watanzania.
Naye Mhandisi Assem Hafez El azar, ambae ni Waziri wa Nyumba Maendeleo ya Makazi na Huduma wa Misri amesema, Serikali ya Misri inawahakikishia watanzania kuwa mradi wa JNHPP ni muhimu kwa nchi zote mbili ili kujenga mahusiano na imani kwa watanzania kuwa misri ni Nchi nyenye uwezo wa kutekeleza miradi mingine mikubwa ambayo Tanzania itatazamia kuijenga.
Katika ziara hiyo Mhe. Makamba aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati, wa Tanzania Mhe. Stephen Byabato, Mkurugenzi wa TANESCO, Maharage Chande pamoja na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati ambao wamekagua pia maeneo muhimu ya mradi yanayoendelea kujengwa ambayo ni nyumba ya mitambo, sehemu ya kupokelea umeme pamoja na eneo linapo jengwa daraja.
Kukamilika kwa wakati kwa mradi Julius Nyerere kutasaidia Nchi kupata umeme wa uhakika, bora na wa gharama nafuu na hivyo kukuza uchumi sambamba na kuongeza ajira kwa wataalamu mbalimbali.