Mkurugenzi wa T – PESA Bi. Lulu Mkunde (kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Kaimu Posta Masta Mkuu Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bw. Aaron Samweli wakitia saini ya makubaliano ya kibiashara kati ya T- PESA na TPC kwa ajili kurahisisha huduma za kifedha kwa mawakala pomoja wateja, hafla hiyo ya kusaini makubaliano imefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TPC.
Mkurugenzi wa T – PESA Bi. Lulu Mkunde (kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Kaimu Posta Masta Mkuu Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bw. Aaron Samweli wakibadilishana mkataba baada ya kutia saini ya makubaliano ya kibiashara kati ya T- PESA na TPC, ambapo TPC anakuwa Wakala Mkuu wa T- PESA kwa ajili kurahisisha huduma za kifedha kwa mawakala pomoja wateja, hafla hiyo ya kusaini makubaliano imefanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TPC.
Kaimu Meneja wa Uhusiano TTCL Bw. Edwin Mashaji akiwa katika majukumu ya kuongoza hafla ya kusaini makubaliano ya kibiashara kati ya T- PESA na TPC iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TPC.
Meneja wa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bw. Amos Millinga akiwa katika hafla ya kusaini makubaliano ya kibiashara kati ya T- PESA na TPC yaliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TPC.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa T – PESA Bi. Lulu Mkunde na Mwakilishi wa Kaimu Posta Masta Mkuu Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bw. Aaron Samweli.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa T – PESA Bi. Lulu Mkunde na Mwakilishi wa Kaimu Posta Masta Mkuu Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bw. Aaron Samweli.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika hafla ya kusaini makubaliano ya kibiashara kati ya T- PESA na TPC yaliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika Ofisi za TPC.
…………………………………………..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) kupitia T- PESA imeingia makubaliano ya kibiashara na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kwa ajili kurahisisha huduma za kifedha kwa mawakala pomoja wateja.
Makunaliano hayo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mpango wa T- PESA kuboresha huduma zake za kifedha nchini kuhakikisha wanawaleta wateja na mawakala karibu ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi, haraka na kwa bei nafuu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kusaini makubaliano ya kibiashara kati ya T – PESA na Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mkurugenzi wa T – PESA Bi. Lulu Mkudde, amesema kuwa Shirika la Posta kwa sasa limebeba dhamana kubwa la kuwahudumia mawakala wadogo pamoja na wateja.
“Tunatambua ukubwa wa shirika la Posta na mchango wake katika kutoa huduma kwa wananchi, tuna imani kuwa wakala mkuu ni chaguo sahihi kwa kuwafikia mawakala wadogo na wateja wote” amesema Bi. Mkudde.
Bi. Mkude amefafanua kuwa muunganiko wa huduma ya kibiashara baina ya taasisi mbili unalenga kuwawezesha wananchi kufanya miamala ya kifedha kwa njia rahisi na salama, kwani wakala wa T – PESA atakuwa na uwezo wa kupata floti kupitia TPC ikiwemo huduma za uwakala na wateja katika kutoa pesa kwenye akaunti zao kupitia ofisi za Posta.
Amesema kuwa makubaliano hayo ya kibiashara yanakwenda kuongeza ufanisi kwa upatikanaji wa huduma za T – PESA, kwani Shirika la Posta litakuwa na jukumu la kuwauzia floti mawakala wadogo kwa ajili ya wao kupeleka huduma sehemu mbalimbali.
“TPC itakuwa inatoa huduma kwa wateja wote wa kawaida katika kutuma na kupokea fedha, tunawafamisha watanzania hivi sasa vocha za TTCL zinapatikana kwenye maduka ya Posta ambayo yanapatikana nchi nzima” amesema Bi. Mkudde.
Bi. Mkudde ameeleza kuwa mpaka sasa takwimu zinaonyesha huduma za kifedha zimewafikia watanzania wengi kwani kupitia simu yake ya mkononi anauwezo wa kutunza na kutumia fedha wakati anaotaka kwa haraka zaidi.
Mwakilishi wa Kaimu Posta Masta Mkuu Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bw. Aaron Samweli, amesema kuwa wakala mkuu wa T- PESA ni fursa, ambapo amehaidi kuwafikia wateja katika maeneo ambayo bado hawajafikiwa na huduma.
Bw. Samweli amesema kuwa watarahisisha upatikanaji huduma za kimtandao kwa kuongeza huduma ya kuweka na kutoa pesa kwa wananchi.
“T -PESA hamjakosea Shirika la Posta kuwa wakala mkuu, ni chaguo sahihi la kuwafikia mawakala wadogo na wateja wote nchi nzima” amesema Bw. Samweli.
Bw. Samweli ametoa wito kwa mashirikia na taasisi mbalimbali kufanya kazi na Shirika la Posta kutokana inarahisisha kuwafikia wananchi wengi zaidi kupitia mtandao wake ulionea nchi nzima.