Dkt.Avelina Mgasa kutoka ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama akiwaonesha wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari waandamizi jinsi damu inavyochakatwa na kuhifadhiwa katika maabara hiyo ya Damu Salama jijini Dar es Salaam..
Mtaalam wa Maabara Farhia Adam akitoa maelezo kwa wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari waandamizi jinsi damu inavyochakatwa na kuhifadhiwa katika maabara hiyo ya Damu Salama.
Dkt.Avelina Mgasa kutoka ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama akitoa mada katika semina ya wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari waandamizi jinsi iliyofanyika kwenye ofisi za Mpango wa Damu Salama Ilala jijini Dar es Salaam leo.
Dkt.Willhelmus Mauka kutoka ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama akitoa mada katika semina hiyo.
Bw. Samwel Mduma Ofisa Viwango na Ubora akifafanua jambo katika semina hiyo.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi wakiwa katika semina hiyo.
Picha ya pamoja.
………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
KUMEKUWA na ongezeko la makusanyo ya chupa za damu kuanzia mwaka 2016 hasa baada ya mpango kuanza kufanya kazi ya ukusanyaji wa damu kwa kushirikiana na timu za halmashauri zote nchini.
Hayo yameemwa leo na Dkt.Willhelmus Mauka kutoka ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama wakati wa mafunzo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali katika kampeni ya ukusanyaji damu kuanzia Desemba 13 hadi 17 jana Dar es Salaam.
Dkt.Mauka amesema kuwa kuna umuhimu wa jamii kuelimishwa juu ya umuhimu wa uchangiaji damu ili kusaidia kufikishwa kiwango cha asilimia 75.
“Kila mwaka mpango hujiweka malengo ya ukusanyaji wa damu ambayo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mpango umeweka malengo ya kukusanya chupa za damu 375,000,” amesema.
Amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la makusanyo ya damu kila mwaka mpaka kufikia mwaka wa fedha 2020/2021 Mpango wa Taifa wa Damu salama ulikusanya jumla ya chupa za zilizokusanywa mwaka 2005 ukilinganisha na chupa za damu 12, 597 zilizokusanywa mwaka 2005 wakati Mpango wa Taifa wa damu kunaanzishwa.
“Kumekuwa na ongezeko la makusanyo ya chupa za damu kuanzia mwaka 2016 hasa baada ya mpango kuanza kufanya kazi ukusanyaji wa damu kwa kushirikiana na timu za halmashauri zote nchini.
Naye Dkt.Avelina Mgasa kutoka ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama amesema kuwa wanatambua kuna changamoto inayofanyika katika hospitali ya uuzwaji damu.
“Jamii inapaswa kutambua kuwa damu haiuzwi na tunaomba ushirikiani pindi inapotokea mtumishi anahitaji pesa inayotokana na mauzo ya damu na kutolwa taarifa kwani mtumishi huyo atakuwa hatarini,” amesema.
Dkt. Avelina amesema kuwa jamii inapaswa kuwa na mwamko wa uchangiaji damu kwani ipo baadhi ya mikoa kama Mkoa wa Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma imekuwa ikifanya vizuri katika uchangiaji wa damu.
“Katika takwimu za Shrika la Afya Duniani (WHO) angalau wastani wa asilimia 1 ya idadi ya watu wanahitajika kuchangia damu na kwa hapa Tanzania watu 10 katika kila watu 1000 wanatakiwa kuchangia damu na kwa sasa inakadiriwa wastani wa watu 550,000 Tanzania wanatakiwa kuchangia damu kwa mwaka,” amesema.