Mdau ambaye ana tatizo la moyo Enelisa Songa akizungumza kabla ya kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya siku ya siku yake ya kuzaliwa Jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mama Mzazi wa mdau ambaye ana tatizo la moyo Nuru Kasaki akielezea namna ambavyo mwanaye amemshangaza kwa kuwakumbuka watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo wakati mdau huyo Enelisa Songa (Kushoto) alipofika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa ikiwa ni ishara ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jana Jijini Dar es Salaam
Msimamizi wa wodi ya watoto ambaye pia ni afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tedy Tarimo akimshukuru Mdau ambaye ana tatizo la moyo Enelisa Songa (kushoto) kwa kujitoa kwake kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye magonjwa ya moyo wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mdau ambaye ana tatizo la moyo Enelisa Songa akimpatia zawadi mbalimbali mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Edina Charles wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mama mzazi wa Mdau ambaye ana tatizo la moyo Nuru Kasaki akimpatia zawadi mbalimbali mama wa mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Latifa Said wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya mwanaye Enelisa Songa (Katikati) Jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Rafiki wa mdau ambaye ana tatizo la moyo Mercy Kobelo akimpatia zawadi mbalimbali mama ambaye mtoto wake amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo Rauhia Rajabu wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yake Enelisa Songa Jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Mdau ambaye ana tatizo la moyo Enelisa Songa akikata keki kwa kushirikiana na baadhi ya watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo wakati wa kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakimlisha keki mdau ambaye ana tatizo la moyo Enelisa Songa kumshukuru kwa zawadi mbalimbali alizowapatia katika kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jana katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Picha na: JKCI
…………………………………………………..
Na: Mwandishi Maalum – Dar es Salaam
Jamii imeombwa iendelee kuwasaidia watoto wenye magonjwa ya moyo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutoa msaada wa mahitaji muhimu kwani watoto hao wanatoka katika maeneo tofauti ya Tanzania na kukaa hospitali muda mrefu hivyo kupata changamoto ya mahitaji yao ya muhimu
Hayo yamesemwa na Msimamizi wa wodi ya watoto ambaye pia ni afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKIC) Tedy Tarimo wakati akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa mdau ambaye ana tatizo la moyo alipofika katika Taasisi hiyo kusherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto waliolazwa JKCI Jana Jijini Dar es Salaam
“Tunamshukuru sana Enelisa pamoja na marafiki zake kwa zawadi walizoleta kwa ajili ya watoto pamoja na mama zao kwa sababu haya ni mahitaji ambayo wagonjwa wetu wanayahitaji, hakika leo ni furaha kwa wagonjwa wetu kupitia zawadi hizi”,
“Upendo uliounesha unatuunganisha kuanzia sasa wewe ni mwenzetu, tunakuombea kwa Mungu changamoto ya tatizo la moyo ulilokuwa nalo liweze kupatiwa matibabu na kuweza kupona kabisa”, alisema Tedy
Aidha Tedy ameiomba jamii kuwafanyia uchunguzi wa afya watoto chini ya miaka 18 mara kwa mara hii itasaidia kugundua kama mtoto ana sumbuliwa na maradhi mapema na kupatiwa huduma za tiba kwa wakati.
“Utakapomfanyia uchunguzi wa afya mwanao na kugundulika na tatizo la moyo ni vyema ukamfikisha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ili aweze kupatiwa matibabu stahiki na kwa wakati kwani mabingwa wa moyo wapo JKCI”, alisema Tedy
Kwa upande wake mdau ambaye ana tatizo la moyo Enelisa Songa alisema katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa aliona ni vyema afike Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani zake kwa watoto wenye matatizo ya moyo kwasababu yeye pia ni mhanga wa ugonjwa huu wa moyo.
“Nimeleta mahitaji mbalimbali ambayo nimejaliwa na mwenyezi Mungu yatakayowasaidia watoto pamoja na mama zao kwani humu wodini kuna wagonjwa ambao wametoka maeneo mbalimbali ikiwemo mikoani na naamini wanahitaji mahitaji haya”,
“Leo nimesindikizwa na marafiki zangu ambao baada ya kusikia kuwa nakuja kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa hawakubaki nyuma nao wakanichangia hivyo mafanikio haya ni pamoja na wao”, alisema Enelisa.
Naye mama mzazi wa mdau ambaye ana tatizo la moyo Nuru Kasaki alikiri kushangazwa na kitendo alichokifanya mtoto wake cha kujitoa kuwasaidia watoto wenye magonjwa ya moyo kwani hakufikiria kuwa ipo siku mwanaye atafanya kitendo alichokifanya katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
“Mwanangu alinipigia simu na kuniomba leo nimsindikize JKCI, nilijua tunakuja kwa ajili ya kliniki zake za kawaida za moyo, kumbe amekuja kunifanyia surprise ya kutoa zawadi kwa watoto, namshukuru Mungu naimani mwanangu atapona”, alisema Nuru