Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geoffrey Mwambe akizungumza katika mkutano uliokutanisha wawekezaji kutoka nchini Misri na wafanyabiashara wa Tanzania kupitia taasisi ya TPSF, Mkutano huo umefanyika kwenye Hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam leo.
……………………………………………………..
Wawekezaji 111 kutoka Cairo nchini Misri wameingia nchini Tanzania kwa ajili ya uwekezàji katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Nishati, ambapo wanatarajia kuanzisha Mji wa Viwanda utakaochukua ekari 500 Kigamboni DSM.
Hatua hiyo inakuja ikiwa zimepita takribani wiki tatu tangu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan afanye ziara ya Kiserikali nchini Misri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geoffrey Mwambe akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam amesema baadhi ya wawekezaji hao pia wataoungana na Rais Samia katika uzinduzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Bidhaa za Umeme Kigamboni.
Waziri Mwambe amesema miongoni mwa wawekezaji atawekeza katika miradi 7 yenye thamani ya U.S.D Bilioni 3.
Naibu Waziri wa NIshati Mh. Steven Biabato akitoa hotuba yake katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam leo.
Injinia Ahmed El Sewedy Electrical Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya El Sewedy Elecrical ya Misri ambaye ameongozana na wawekezaji wennzake kutoka nchini Misri kuja kuona fursa za uwekezaji nchini.
Mohammed Abdel Wahab Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwekezaji Misri (GAFI) akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Rengency jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geoffrey Mwambe na Naibu Waziri wa NIshati Mh. Steven Biabato wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam leo.
Picha mbalimbali zikionesha wawekezajimbalimbali kutoka nchini Misri wakiwa katika mkutano uliofanyika leo kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es Salaam leo.