Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango,akiwasili katika Kituo cha kulelea yatima cha Rahman Orphanage Centre kilichopo Chang’ombe jijini Dodoma kwa ajili ya kutoa misaada ya vitu mbalimbali tukio hilo limefanyika leo Desemba 4,2021.
Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango,akizungumza katika Kituo cha kulelea yatima cha Rahman Orphanage Centre kilichopo Chang’ombe jijini Dodoma kabla ya kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali katika kituo hicho leo Desemba 4,2021.
Mwenyekiti wa Capital City Women Group na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Tunu Pinda,akielezea jinsi walivyoguzwa mpaka kuja kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Kituo cha kulelea yatima cha Rahman Orphanage Centre kilichopo Chang’ombe jijini Dodoma leo Desemba 4,2021.
Katibu Msaidizi wa Kituo cha kulelea yatima cha Rahman Orphanage Centre kituo hicho, Abdallah Said,akisoma risala kwa viongozi hao waliofika kutoa misaada ya vitu mbalimbali leo Desemba 4,2021.
Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Rahman Orphanage Centre kilichopo Chang’ombe jijini Dodoma wakifatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi waliotembelea na kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali leo Desemba 4,2021.
Muonekano wa vitu mbalimbali vya msaada vilivyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Capital City Women Group na Women Federation for World Peace kwenye kituo cha Rahman Orphanage Centre kilichopo Chang’ombe jijini Dodoma
Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na watoto mara baada ya kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali katika Kituo cha kulelea yatima cha Rahman Orphanage Centre kilichopo Chang’ombe jijini Dodoma leo Desemba 4,2021.
Sista Asella Michael,akisoma risala ya kituo cha Nyumba ya Basiliana ya Shirika la Masista wa St. Gema mara baada ya viongozi kutembelea kituo hicho pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali.
Masista wa kituo cha Nyumba ya Basiliana wakipokea vitu mbalimbali vya msaada vilivyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Capital City Women Group na Women Federation for World Peace katika kituo hicho.
Masista wazee waliopo katika kituo cha Nyumba ya Basiliana ya Shirika la masista wa St. Gema wakisikiliza risala mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kituo hicho.
Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango,akikawakabidhi misaada ya vitu mbalimbali Masista wazee waliopo katika kituo cha Nyumba ya Basiliana ya Shirika la masista wa St. Gema vilivyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Capital City Women Group na Women Federation for World Peace katika kituo hicho jijini Dodoma leo Desemba 4,2021.
Mhuduma wa kituo cha Nyumba ya Basiliana ya Shirika la Masista wa St. Gema Sista Salome Augustino,akitoa neno la shukrani baada ya kupokea misaada ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Capital City Women Group na Women Federation for World Peace katika kituo hicho leo Desemba 4,2021 jijini Dodoma.
Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi baada ya kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali katika kituo cha Nyumba ya Basiliana ya Shirika la masista wa St. Gema kinachotunza Masista Wazee na wagonjwa vilivyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Capital City Women Group na Women Federation for World Peace katika kituo hicho jijini Dodoma leo Desemba 4,2021.
………………………………………………………………..
Na Alex Sonna, Dodoma
VITUO viwili vya kulelea wazee na watoto yatima jijini Dodoma vimepatiwa misaada vitu mbalimbali ikiwamo vyakula vyenye thamani ya Sh.Milioni 10.6.
Msaada huo umetolewa leo Desemba 4,2021 jijini Dodoma na Ofisi ya Makamu wa Rais, Capital City Women Group na Women Federation for World Peace kwenye kituo cha Nyumba ya Basiliana ya Shirika la masista wa St. Gema inayotunza masista wazee na wagonjwa na Kituo cha kulelea yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe jijini hapa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango, amesema kuwajali wahitaji ni miongoni mwa mambo ya msingi ili kupunguza changamoto zinazowakabili watu hao wenye mahitaji.
“Kuna watu wanakesha kutuombea kwa ajili yetu kama Masista na sisi kwenye Umoja wetu tukaona lazima tufanye jambo tuweze kuleta kile kidogo ambacho kitasaidia katika changamoto,” amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Capital City Women Group na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Tunu Pinda ametoa wito kwa jamii na wadau mbalimbali kuwasaidia watu wenye mahitaji ili kuondokana na changamoto zinazowakabili.
Ametaja vitu vilivyotolewa kwa vituo hivyo ni mchele,unga, mafuta ya kupikia, maharage, Sabuni dawa ya mswaki ,vitenge, khanga pamoja na fedha taslimu,
Awali katika risala yao ya nyumba ya Basiliana, Sista Asella Michael, amesema nyumba hiyo inatunza masista wazee na wagonjwa 35.
Amesema Masista wa nyumba ya Basiliana kutokana na hali zao za kiafya wamekuwa na mahitaji maalum ikiwemo lishe bora na matibabu na wengine wamelazwa Hospitali ya St. Gema kutokana na matatizo mbalimbali ya kiafya.
Aidha amesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya maji na uchakavu wa miundombinu na mipango yao ya baadae ni kuboresha miradi ya kilimo na ufugaji.
Katika risala ya Kituo cha Rahman Orphanage Centre, Katibu Msaidizi wa kituo hicho, Abdallah Said amesema kuna yatima 45 wanaoishi bweni na 70 wanaoishi na walezi wao.
Amesema wamepata eneo lingine lenye ukubwa wa mita za mraba 20,521 lengo ni kuanzisha Chuo cha Ufundi Stadi na inahitajika gharama za upimaji na umilikishwaji kiasi cha Sh.milioni 104.5.