Home Michezo WAZIRI BASHUNGWA AWAPONGEZA TANZANITE KWA KUIBUKA WASHINDI DHIDI YA BURUNDI

WAZIRI BASHUNGWA AWAPONGEZA TANZANITE KWA KUIBUKA WASHINDI DHIDI YA BURUNDI

0

**************************

Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 Tanzinite imeibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya timu ya Burundi katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa leo Desemba 4, 2021 katika uwanjwa wa Chamanzi jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amewapongeza wachezaji wa timu hiyo ya Taifa ambapo alikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza uwanjani hapo kuwapa hamasa na kuwafanya waibuke kidedea kwa ushindi mnono.

Waziri Bashungwa ametumia fursa hiyo kuwapongeza wachezaji pamoja na kamati ya ufundi ambapo amesema wameitendea haki fursa ya kutumia uwanja wa nyumbani na kuibuka washindi.

Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo mbili unatarajiwa kuchezwa Desemba 18 nchini Burundi kwa timu ya Tanzanite kuwa na faida ya pointi tatu kibindoni.