Baadhi ya wananchi wakiwa katika maadhinino hayo wilayani Ruangwa.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika maadhinino hayo wilayani Ruangwa.
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bw. Hassan Ngoma akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya siku ya Siku ya Ukimwi iliyofanyia wilayani humo leo.
Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma amewataka wananchi kuacha mara moja tabia ya kuwanyanyapa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi kwa sababu ugonjwa huo hautokani na matakwa ya kibinadamu.
Mhe. Ngoma amesema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya ukimwi kitaifa yaliyofanyika kiwilaya kijiji cha Chinokolo leo 01/12/2021 ambapo amesema kuwa hakuna anayeweza kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kukaa na mtu sehemu moja, kula pamoja au kushirikiana naye katika kufanya kazi za kuongeza kipato.
“Msiwanyayapae waathirika Huwezi kupata maambukizi kwa kushikana mikono na mtu watu wenye maambukizi wanahaki kama walivyo wasio na maambukizi” Amesema Mhe. Ngoma.
Aidha amebainisha kuwa ni muhimu watu kuendelea kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kuwakinga wengine kwani ukimwi upo na unaua.
“Kumekuwa na kauli za Ukimwi ni ugonjwa wa kawaida kama yalivvyo malaria au mafua kauli hizi zinachochea maambukizi nawakumbusha ukimwi upo jaman na unatisha tuache kuchukulia poa mlinde na mkinge umpendae na ukimwi haupimwi kwa macho usimuone mtu
amenona ukaona huyu anakufaa bila kupima huwezi jua huyu anakufaa au la acheni kuangalia kwa macho macho si kipimo sahihi kipo kipimo sahihi nendeni kwenye zahanati zenu mkapime” Amesema Mhe. Ngoma
Mhe. Ngoma amesisiziza watoto ambao ni yatima na wamepata maambukizi kutoka kwa wazazi wao na kwa sasa wanaishi na watu wengine wahamasishwe kwenda kuchukua dawa kwa wakati.
Katika hatua nyingine Mhe. Ngoma amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa watakaokuwa wanafanya sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kuanza mwakani mwezi Agosti.
Pia amewataka wananchi kuendelea kujikinga na ugonjwa wa corona na kuendelea kufuata masharti yote yaliyowekwa na kwenda kupata chanjo kama inavyoelekezwa na serikali.
“Acheni kusikiliza maneno ambayo hayana ukweli ndani yake kuwa ukichanjwa unapata madhara baadae nendeni mkapate chanjo ili mzidi kujikinga” Amesema Mhe.Ngoma.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Mikidadi Mbute ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti Ukimwi amewataka waganga wa kienyeji kutoa tiba zao kwa kufuata utaratibu na si kuwarundika wananchi katika eneo moja.
Mhe. Mbute amesema Kuna baadhi ya waganga wanatabia za kutoa tiba kwa kuweka watu wengi katika maeneo yao na kutoa dawa kwa vifaa ambavyo wanatumia mtu zaidi ya mmoja jambo linaloweza kusababisha mlipuko wa magonjwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
“Mganga mkuu fanya kupita katika hayo maeneo uone mtoe elimu kwa watoa tiba na wapokea tiba ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi katika wilaya yetu” Amesisitiza Mhe. Mbute.
Kilele cha Maadhimisho ya siku ukimwi duniani kimefanyika kiwilaya katika kata ya Makanjiro kijiji cha Chinokole huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ikiwa ni “Zingatia usawa tokomeza ukimwi tokomeza magonjwa ya mlipuko”.
MWISHO