Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel G. Chongolo (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam.
Katika picha ya pamoja, Katibu Mkuu wa CCM Daniel G. Chongolo (kushoto), Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Chen Mingjian (katikati) na kulia ni Katibu Wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali (mst) Ngemela Lubinga mara baada ya kumaliza mazungumzo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Lumumba Jijini Dar es salaam.(Picha na CCM Makao Makuu
……………………………………………………………..
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) Ndg. Daniel G Chongolo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Chen Mingjian.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 01 Disemba, 2021 katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu Lumumba Jijini Dar Es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yamelanga katika kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa baina ya nchi mbili za Tanzania na China kupitia vyama tawala vya CCM na CPC.