Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli kuanzia leo ,Mkurugenzi wa Petroli  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw.Gerald Maganga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu bei Kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli zilizoanza kutumika leo Desemba 1,2021.Kushoto kwake ni Meneja Biashara wa Petroli EWURA Bi.Kemilembe Kafanabo

……………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetaja bei mpya za mafuta kwa mwezi Desemba mwaka 2021 ambapo  imesema   mafuta ya petroli, bei itakuwa Shilingi 2,510 kwa lita kwa Dar es Salaam, huku Tanga na Mtwara bei itakuwa Shilingi 2,525 kwa lita na Shilingi 2,569 kwa lita, mtawalia.

Imesema kwa mafuta ya dizeli, bei itakuwa Shilingi 2,392 kwa lita kwa Dar es Salaam, wakati Tanga na Mtwara bei itakuwa Shilingi 2,413 kwa lita na Shilingi 2,423 kwa lita, mtawalia.

Imesema  kwa mafuta ya taa, bei itakuwa Shilingi 2,235 kwa lita kwa Dar es Salaam na bei za bidhaa hiyo kwa mikoa yote nchini zimekokotolewa kwa kujumuisha gharama za usafirishaji mpaka miji husika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli kuanzia leo ,Mkurugenzi wa Petroli  EWURA,Bw.Gerald Maganga amesema bei ya mafuta ya petroli, itakuwa Shilingi 2,510 kwa lita kwa Dar es Salaam, huku Tanga na Mtwara bei itakuwa Shilingi 2,525 kwa lita na Shilingi 2,569 kwa lita, mtawalia.

Amesema kwa mafuta ya dizeli, bei itakuwa Shilingi 2,392 kwa lita kwa Dar es Salaam, wakati Tanga na Mtwara bei itakuwa Shilingi 2,413 kwa lita na Shilingi 2,423 kwa lita, mtawalia.

Bw.Maganga amesema  kwa mafuta ya taa, bei itakuwa Shilingi 2,235 kwa lita kwa Dar es Salaam na bei za bidhaa hiyo kwa mikoa yote nchini zimekokotolewa kwa kujumuisha gharama za usafirishaji mpaka miji husika.

Maganga amesema bei ya petroli imeongezeka kwa asilimia 23 kutoka dola za Marekani 644.01 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 793.14 kwa tani mwezi Oktoba 2021.

Amesema Kwa kipindi hicho, bei ya petrol katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 241 kwa lita na kufikia Shilingi 2,610 kwa lita mwezi Desemba 2021.

Bw.Maganga amesema bei ya dizeli imeongezeka kwa asilimia 30 kutoka dola za Marekani 550.68 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 713.28 kwa tani mwezi Oktoba 2021.

Amesema Kwa kipindi hicho, bei ya dizeli katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 311 kwa lita na kufikia Shilingi 2,492 kwa lita mwezi Desemba 2021.

Amesema  bei za mafuta ya taa imeongezeka kwa asilimia 30 kutoka dola za Marekani 558.90 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 726.56 kwa tani mwezi Oktoba 2021.

Aidha Maganga amesema kwa kipindi hicho, bei ya mafuta ya taa katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 120 kwa lita na kufikia Shilingi 2,235 kwa lita mwezi Desemba 2021.

Maganga amesema kwa lengo la kupungu ongezeko la bei za mafuta hapa nchini, Serikali ilifanya juhudi za makusudi ambapo tarehe 5 Oktoba 2021, Serikali ilipunguza tozo mbalimbali za taasisi zake kwa kiwango cha Shilingi 29.38 kwa lita ya petroli, Shilingi 30.05 kwa lita ya dizeli na Shilingi 26.99 kwa lita ya mafuta ya taa.

Amesema pamoja na juhudi hizo, Serikali imeendelea kuchukua hatua zaidi kutokana na kuendelea kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia.

“Hivyo, kwa mwezi Desemba 2021, Serikali imeahirisha kukusanya Ada ya Mafuta(Petroleum fee) ya Shilingi 100 kwa lita kwenye mafuta ya petroli na dizeli,”amesema.

Pia amesema kulingana na mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia, bei za mwezi Novemba 2021 zimeanza kushuka.

“Kwakuwa bei za soko la dunia zinaakisiwa katika soko la hapa nchini baada ya miezi miwili, unafuu wa bei za soko la dunia ulioanza kujitokeza katika mwezi Novemba 2021 unatarajiwa kuonekana katika soko la hapa nchini katika bei za mwezi Januari 2022,”amesema.

Amesema Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na kufanya kila linalowezekana ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza katika mnyororo mzima wa uchumi hapa nchini iwapo bei zitaongezeka kwa kiwango kikubwa.

 

JEDWALI A: BEI ZA REJAREJA

MjiBei Kikomo
Petroli 

(Shilingi/Lita)

Dizeli 

(Shilingi/Lita)

Mafuta Ya Taa (Shilingi/Lita)
Dar es Salaam 2,510 2,392 2,235
Arusha 2,582 2,470 2,319
Arumeru (Usa River) 2,582 2,470 2,319
Karatu 2,600 2,488 2,338
Longido 2,593 2,481 2,330
Monduli 2,587 2,475 2,325
Monduli-Makuyuni 2,592 2,480 2,330
Ngorongoro (Loliondo) 2,666 2,554 2,411
Coast (Kibaha) 2,515 2,396 2,240
Bagamoyo 2,521 2,403 2,246
Bagamoyo (Miono) 2,552 2,434 2,277
Chalinze Junction 2,524 2,406 2,249
Chalinze Township (Msata) 2,529 2,410 2,254
Kibiti 2,531 2,412 2,256
Kisarawe 2,517 2,399 2,242
Mkuranga 2,520 2,402 2,245
Rufiji 2,538 2,420 2,263
Dodoma 2,569 2,451 2,294
Bahi 2,576 2,458 2,301
Chamwino 2,564 2,446 2,289
Chemba 2,595 2,477 2,321
Kondoa 2,602 2,484 2,327
Kongwa 2,566 2,448 2,291
Mpwapwa 2,570 2,452 2,295
Mpwapwa (Chipogoro) 2,582 2,464 2,307
Mtera (Makatopora) 2,588 2,470 2,313
Mvumi 2,576 2,457 2,301
Geita 2,676 2,557 2,401
Bukombe 2,665 2,546 2,390
Chato 2,697 2,578 2,422
Mbogwe 2,714 2,595 2,439
Nyang’hwale 2,691 2,572 2,416
Iringa 2,574 2,456 2,299
Ismani 2,580 2,461 2,305
Kilolo 2,579 2,460 2,304
Mufindi (Mafinga) 2,584 2,466 2,309

4 

MjiBei Kikomo
Petroli 

(Shilingi/Lita)

Dizeli 

(Shilingi/Lita)

Mafuta Ya Taa (Shilingi/Lita)
Mufindi (Igowole) 2,593 2,475 2,318
Kagera (Bukoba) 2,726 2,607 2,451
Biharamulo 2,700 2,582 2,425
Karagwe (Kayanga) 2,742 2,624 2,467
Kyerwa (Ruberwa) 2,748 2,630 2,473
Muleba 2,726 2,607 2,451
Ngara 2,714 2,595 2,439
Misenyi 2,734 2,616 2,459
Katavi (Mpanda) 2,718 2,600 2,443
Mlele (Inyonga) 2,738 2,619 2,463
Mpimbwe (Majimoto) 2,711 2,593 2,436
Tanganyika (Ikola) 2,736 2,618 2,461
Kigoma 2,742 2,623 2,467
Uvinza (Lugufu) 2,754 2,636 2,479
Buhigwe 2,731 2,613 2,456
Kakonko 2,699 2,580 2,424
Kasulu 2,728 2,609 2,453
Kibondo 2,706 2,588 2,431
Kilimanjaro (Moshi) 2,571 2,459 2,309
Hai (Bomang’ombe) 2,574 2,462 2,312
Mwanga 2,564 2,452 2,302
Rombo (Mkuu) 2,588 2,476 2,330
Same 2,558 2,445 2,295
Siha (Sanya Juu) 2,578 2,466 2,316
Lindi 2,583 2,436 2,294
Lindi-Mtama 2,587 2,441 2,312
Kilwa Masoko 2,606 2,460 2,269
Liwale 2,618 2,472 2,315
Nachingwea 2,602 2,456 2,323
Ruangwa 2,609 2,463 2,325
Manyara (Babati) 2,616 2,504 2,358
Hanang (Katesh) 2,626 2,514 2,368
Kiteto (Kibaya) 2,631 2,519 2,369
Mbulu 2,628 2,516 2,371
Simanjiro (Orkasumet) 2,648 2,536 2,390
Mara (Musoma) 2,689 2,571 2,414
Musoma Vijijini (Busekela) 2,730 2,611 2,455
Rorya (Ingirijuu) 2,698 2,579 2,423
Rorya (Shirati) 2,733 2,614 2,458
Bunda 2,680 2,562 2,405
Bunda (Kisorya) 2,690 2,571 2,415
Butiama 2,686 2,567 2,411

5

MjiBei Kikomo
Petroli 

(Shilingi/Lita)

Dizeli 

(Shilingi/Lita)

Mafuta Ya Taa (Shilingi/Lita)
Serengeti (Mugumu) 2,735 2,616 2,460
Tarime 2,700 2,582 2,425
Tarime (Kewanja/Nyamongo) 2,704 2,586 2,430
Mbeya 2,617 2,499 2,342
Chunya 2,627 2,509 2,352
Chunya (Makongolosi) 2,632 2,514 2,357
Chunya (Lupa Tingatinga) 2,634 2,516 2,359
Kyela 2,633 2,515 2,358
Mbarali (Rujewa) 2,601 2,483 2,327
Rujewa (Madibira) 2,615 2,496 2,340
Rujewa (Kapunga) 2,611 2,493 2,336
Rungwe (Tukuyu) 2,626 2,508 2,351
Morogoro 2,535 2,417 2,260
Mikumi 2,551 2,433 2,276
Kilombero (Ifakara) 2,573 2,455 2,298
Kilombero (Mlimba) 2,595 2,477 2,321
Kilombero (Mngeta) 2,585 2,466 2,310
Ulanga (Mahenge) 2,584 2,465 2,309
Malinyi 2,594 2,476 2,319
Kilosa 2,554 2,435 2,279
Gairo 2,554 2,435 2,279
Mvomero (Wami Sokoine) 2,546 2,427 2,271
Mvomero (Sanga Sanga) 2,535 2,417 2,260
Turian 2,560 2,442 2,285
Mtwara 2,569 2,423 2,308
Nanyumbu (Mangaka) 2,605 2,459 2,357
Masasi 2,585 2,439 2,333
Newala 2,590 2,444 2,340
Tandahimba 2,583 2,437 2,333
Nanyamba 2,583 2,437 2,333
Mwanza 2,660 2,542 2,385
Kwimba 2,678 2,560 2,403
Magu 2,668 2,550 2,394
Misungwi 2,655 2,536 2,380
Sengerema 2,693 2,575 2,418
Ukerewe 2,720 2,602 2,445
Njombe 2,603 2,484 2,328
Njombe (Kidegembye) 2,623 2,505 2,348
Ludewa 2,641 2,522 2,366
Makambako 2,595 2,477 2,320
Makete 2,634 2,515 2,359
Wanging’ombe (Igwachanya) 2,600 2,482 2,326

6

MjiBei Kikomo
Petroli 

(Shilingi/Lita)

Dizeli 

(Shilingi/Lita)

Mafuta Ya Taa (Shilingi/Lita)
Rukwa (Sumbawanga) 2,683 2,565 2,408
Sumbawanga Rural (Mtowisa) 2,683 2,565 2,408
Kalambo (Matai) 2,690 2,572 2,415
Nkasi (Namanyele) 2,697 2,578 2,422
Ruvuma (Songea) 2,655 2,508 2,359
Mbinga 2,667 2,521 2,392
Namtumbo 2,646 2,499 2,388
Nyasa (Mbamba Bay) 2,692 2,546 2,403
Tunduru 2,620 2,474 2,418
Shinyanga 2,640 2,521 2,365
Kahama 2,653 2,535 2,378
Kishapu 2,668 2,549 2,393
Ushetu (Nyamilangano) 2,670 2,552 2,395
Ushetu (Kangeme Village) 2,661 2,543 2,386
Salawe 2,654 2,536 2,379
Simiyu (Bariadi) 2,681 2,562 2,406
Busega (Nyashimo) 2,674 2,555 2,399
Itilima (Lagangabilili) 2,684 2,565 2,409
Maswa 2,672 2,554 2,397
Meatu (Mwanhuzi) 2,679 2,561 2,404
Singida 2,601 2,483 2,326
Iramba 2,613 2,495 2,338
Manyoni 2,586 2,467 2,311
Itigi (Mitundu) 2,601 2,483 2,326
Ikungi 2,596 2,478 2,322
Mkalama (Nduguti) 2,626 2,507 2,351
Songwe (Vwawa) 2,627 2,508 2,352
Songwe (Mkwajuni) 2,634 2,515 2,359
Ileje 2,631 2,512 2,356
Momba (Chitete) 2,636 2,517 2,361
Tunduma 2,631 2,512 2,356
Tabora 2,618 2,500 2,344
Igunga 2,618 2,500 2,343
Kaliua 2,632 2,513 2,357
Ulyankulu 2,629 2,511 2,354
Nzega 2,629 2,511 2,354
Sikonge 2,627 2,509 2,352
Urambo 2,628 2,510 2,353
Uyui 2,625 2,506 2,350
Mpyagula 2,650 2,532 2,375
Tanga 2,525 2,413 2,281
Handeni 2,546 2,433 2,261

7

MjiBei Kikomo
Petroli 

(Shilingi/Lita)

Dizeli 

(Shilingi/Lita)

Mafuta Ya Taa (Shilingi/Lita)
Kilindi 2,561 2,448 2,295
Korogwe 2,537 2,425 2,274
Lushoto 2,546 2,434 2,284
Mkinga (Maramba) 2,532 2,420 2,296
Muheza 2,530 2,418 2,281
Pangani 2,532 2,420 2,288

JEDWALI B: BEI ZA JUMLA 

Petroli  

(Shilingi/Lita)

Dizeli  

(Shilingi/Lita)

Mafuta ya Taa  (Shilingi/Lita)
DAR ES SALAAM 2,380.36 2,262.03 2,106.51
TANGA 2,395.03 2,282.95
MTWARA 2,438.96 2,292.91