*************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo wao ligi ya NBC dhidi ya Mbeya Kwanza kwa kufanikiwa kuwanyuka mabao 2-0.
Mchezo huo ambao umepigwa kwenye dimba la Sokoine Mbeya, Yanga iliwapumzisha wachezaji wao kadhaa na kuweza kuwapa nafasi wachezaji wengine kama Brison,Mauya na Ntibazokiza.
Said Ntabazokiza aliza kuiandikia bao timu yake ya Yanga mara baada ya kupiga faulu ya moja kwa moja na kutinga nyavuni mara baada ya Feisal Salumu kuchezewa rafu nje kidogo ya kumi na nane.
Bao la pili lilifungwa na Fiston Mayele ambaye alifunga bao hilo na kwenda mpaumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao mawili mbele ya Mbeya Kwanza ambao walikuwa nyumbani.
Mpaka mpira unamalizika Yanga aliibuka na ushindi wa mabao 2-0 licha ya kipindi cha pili kuzidiwa na Mbeya Kwanza ambao walikuwa wanalisakama lango la Yanga bila mafanikio.
Yanga sasa itakaa siku kumi wakijiandaa kumenyana na wapinzani wao Simba Sc mchezo ambao utapigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Disemba 11,2021.