Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo kutoka Taasisi mahiri ya utafiti nchini Tanzania (REPOA ) Dkt Lucas Katera wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari
hizi katika ofisi za Taasisi hiyo.
…………………………………..
NA
MUSSA KHALID,
Imeelezwa
kuwa tafiti zinaonyesha ni vizuri kujenga mazingira ya kuwavutia wawekezaji
nchini waweze kujenga ili kusaidia uzalishaji na hivyo kukuza uchumi wa nchi na
kuondokana na umaskini.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na
Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo kutoka Taasisi mahiri ya utafiti nchini Tanzania (REPOA ) Dkt Lucas Katera
wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi kuhusu umuhimu na mchango
wa utafiti katika maendeleo ya nchi.
Dkt Katera
amesema kuwa REPOA inashughulika na ufanyaji wa tafiti mbalimbali ikiwemo
kujenga uwezo na kusaidia katika utungaji wa sera katika Nyanja za ukuaji wa
uchumi,pamoja na jinsia katika jamii kuhusu namna ya kunufaika na uchumi.
Amesema
kuwa ni vyema utafiti ukapewa nafasi katika kutengeneza mipango ya maendeleo
kwani itasaidia kuleta matokeo mazuri katika ukuaji wa nchi.
Aidha Dkt Katera amesema katika utafiti mfaidika mkubwa katika matokeo yake ni serikali
pamoja na sekta binafsi kwani unasaidia kuibua changamoto mbalimbali za
kusaidia kukua zaid.
Katika
Hatua nyingine kuelekea miaka 60 ya Uhuru Mkurugenzi huyo wa tafiti na mafunzo
REPOA amesema tafiti zimajaribu kutatua matatizo na kuweza kuyatatua yakiwemo
ya huduma za jamii kama ajira,elimu na afya.
Hata
hivyo ameiomba serikali kuendelea
kuonyesha mchango katika utafiti ikiwa ni pamoja na kuweka bajeti maalum ambayo
itazisaidia taasisi hizo kuwa na rasilimali fedha zitakazowasaidia kufanyia
tafiti zao.