
****************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Wadau wa usafirishaji nchini wametakiwa kuwa makini na kujali maisha yao na wenzao pindi wanapokuwa wakitumia vyombo vya moto barabarani.
Hayo yamesemwa na Meneja Vilainishi kutoka kampuni ya Puma Lubricants inayohusika na uuzaji wa bidhaa za mafuta ya Puma Energy ,Prosper Kasenegala wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Amesema kuwa, wamekuwa wakishirikiana na jeshi la polisi katika kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya barabarani sambamba na kuuza bidhaa zilizo bora za Vilainishi vya magari ambavyo vikitumiwa gari linakuwa salama na unakuwa na uhakika wa safari yako.
Prosper ameongeza kuwa,wamekuwa wakisisitiza juu ya usalama mkuu kwa watumiaji wa barabara ili kuepuka ajali za barabarani kwani ajali zinapotokea kunakuwa na majeruhi na kukiwa na majeruhi wengi kuna sababisha kazi kutetereka na kupunguza nguvu kazi ya nchi.
“bidhaa hii tumeleta kwa ajili ya mahitaji ya watumiaji ya watu kwani ni bidhaa bora na sahihi kwa matumizi na usalama wa barabarani na inasaidia Sana kupunguza ajali za barabarani.”amesema .
Amesema kuwa, kampuni hiyo imekuja na bidhaa mpya ya Vilainishi ambayo wateja wake wameshaanza kuitumia tayari huku akiwataka wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuitumia bidhaa hiyo mpya ambayo ina ubora wa hali ya juu.
Naye Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja kutoka shirika la bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule amesema kuwa, wameshiriki katika maonyesho hayo wakiwa kama wadau kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali .
Amewataka wadau hao kuhakikisha wanatembelea banda lao na kuweza kupata elimu juu ya maswala ya bima huku akiwataka kukatia bima magari yao kwa ajili ya usalama wao na mali zao.