Afisa Mwandamizi Biashara wa Benki ya Maendeleo TIB, Adam Athuman (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Benki hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa wa Benki ya Maendeleo TIB, Adam Athuman (kushoto) na Giusy Mbolile (katikati) wakimsikiliza kwa makini mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la Benki hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Kitaasisi wa benki hiyo, Saidi Mkabakuli (kulia) akitoa ufafanuzi wa mikopo na huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa mmoja wa washiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba akipata maelezo kuhusu Benki ya Maendeleo TIB kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Kitaasisi wa benki hiyo, Saidi Mkabakuli (kulia) wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba akitoa maelekezo kwa Meneja Masoko na Uhusiano wa Kitaasisi wa Benki ya Maendeleo TIB, Saidi Mkabakuli (kulia) wakati alipotembelea Banda la Benki hiyo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Charles Mwamwaja.
……………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu,
Benki ya Maendeleo TIB imeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 8 mpaka 14 Novemba.
Benki ya Maendeleo TIB imeshiriki katika Maadhimisho hayo kwa lengo la kutoa uelewa na kuwafikia wananchi kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya hayo, Meneja Masoko na Uhusiano wa Kitaasisi wa benki hiyo, Bw. Saidi Mkabakuli amesema benki hiyo imeshiriki katika maadhimisho hayo ili kutoa kuelimisha umma kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na benki kwa wadau na wananchi wanaotembelea maadhimisho hayo.
“Tukiwa moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, tumeshiriki katika maadhimisho haya ili kuwafikia wananchi na kuwaelimisha na kuongeza uelewa wa wananchi juu ya manufaa ya huduma za kifedha ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
Aliongeza kuwa benki imetumia maadhimisho hayo kwa ajili ya kusambaza taarifa na kujua mitazamo, kero na mahitaji ya taarifa za wadau wa benki hiyo ili kuiwezesha kuimarisha bidhaa na huduma zake.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa Mwaka 2020/21 – 2029/30 kupitia elimu kwa umma.
Wiki ya Huduma za Fedha inalenga kuwafikia wadau mbalimbali wakiwemo: watumishi wa umma; wanafunzi; wakufunzi; wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu; wajasiriamali wadogo na wa kati (MSMEs); asasi za kiraia; Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari; watoa huduma za fedha; watoto na umma kwa ujumla.