Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa Benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi akipokea tuzo kutoka kwa Shelryar Ali Meneja Mkazi wa Mastercard International Afrka Mashariki inayoitambua benki hiyo kwa juhudi zake za kukuza matumizi ya Mastercard nchini katika hafla iliyofanyika Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa Benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi akionesha tuzo hiyo mara baada ya kuipokea kutoka kwa Shelryar Ali kushoto Meneja Mkazi wa Mastercard International Afrka Mashariki inayoitambua benki hiyo kwa juhudi zake za kukuza matumizi ya Mastercard nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa Benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi na Shelryar Ali Meneja Mkazi wa Mastercard International Afrka Mashariki wakionesha tuzo inayoitambua benki hiyo kwa juhudi zake za kukuza matumizi ya Mastercard nchini mara baada ya kukabidhiana kushoto ni Victor Ndlovu Mkuu wa Maendeleo ya Biashara Mastercard International Afrika Mashariki na Kulia ni Bw. Filbert kutoka NMB
Picha ya pamoja
………………………………………
Benki ya NMB imepokea tuzo kubwa kutoka kwa Mastercard International inayoitambua benki hiyo kwa juhudi zake za kukuza matumizi ya Mastercard nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa Benki ya NMB Bw. Filbert Mponzi wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akipokea tuzo ya Mastercard International Afrka Mashariki inayoitambua benki hiyo kwa juhudi zake za kukuza matumizi ya Mastercard nchini.
“Ni furaha kubwa kwa benki ya NMB kupokea tuzo kutoka kwa washirika wetu wa Kibenki – Mastercard kwa kutambua kuwa NMB ni benki kinara na ya kwanza katika kukuza matumizi ya kadi kwa kasi kubwa sana nchini Tanzania.” Amesema Mponzi.
Amesema tuzo hiyo ni kielelezo tosha kabisa cha ukubwa wa benki ya NMB nchini inayochagizwa na upana wa mtandao wake wa matawi 226 na wateja Zaidi ya Milioni 4. Hii ni tuzo ya kwanza ya namna hii kuwahi kutolewa kwa benki hapa nchini Tanzania.
Aidha amewashukuru Mastercard International kwa tuzo hyo lakini zaidi wateja wa NMB walioifanya pakubwa kuwezesha benki hiyo kubwa nchini kutambuliwa na Mastercard na hatimaye kupewa tuzo.
“Benki ya NMB imepata tuzo hii kwa sababu ya Idadi kubwa zaidi ya wateja wanaotumia kadi kuliko benki yoyote nchini. Zaidi ya wateja wa NMB milioni 3 wanatumia kadi za Mastercard kwaajili ya huduma mbalimbali za kifedha na hii ni idadi kubwa zaidi kufikiwa na benki yeyote nchini.” Amesema Mponzi.
Ameainisha sababu nyingine kuwa ni Kiasi kikubwa cha pesa kilichotumika katika vituo vya mauzo yaani POS , Malipo mbalimbali kwa kutumia kadi za NMB MasterCard na ndio kiasi kikubwa kuliko benki yeyote hapa nchini huku kikikua kwa asilimia 104 ndani ya mwaka mmoja.
Ameongeza kuwa mbali na sababu hizi, benki ya NMB imekuwa kinara katika kuhamasisha matumizi ya kadi ya benki sio tu kwa ajili ya kutolea pesa katika ATM bali katika matumizi mbalimbali kama kufanya malipo katika sehemu za migahawa, supermarket, vituo vya mafuta na hata katika sehemu za starehe hata kuagiza bidhaa mbalimbali kupitia mitandao. ambapo ukitumia kadi za NMB Mastercard, usalama wake ni wa hali ya juu.
“Ni imani yangu mmekuwa mkikutana na matangazo mbalimbali ya NMB kuhimiza malipo kwa kadi na hata mmekuwa mkiona promosheni mbalimbali kama NMB FRIYAY na MASTABATA ambazo zote zinalenga kuhamasisha malipo kwa kutumia kadi.” Amesema Bw. Mponzi.
Ameongeza kuwa Benki ya NMB itaendelea kubuni suluhisho mbalimbali zenye lengo la kuboresha matumizi ya kadi na kwa kutumia teknolojia mbalimbali, huduma hizi zitazidi kuwa bora Zaidi.
Amemaliza kwa kusema ni fahari kwa benki ya NMB, kufanya kazi na Mastercard kwani teknolojia na ubobezi wao katika matumizi ya malipo kwa kadi ni bora na unaotambulika ulimwenguni kote. Hii imerahisisha utoaji wa huduma na kuwa na msaada mkubwa kwa wateja wetu.