Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa.
……………………………………………
Mawakili 20 kutoka mkoa wa Njombe na Iringa wanatarajiwa kutoa msaada wa kisheria siku tatu mfululizo kwa wananchi wa wilaya ya Njombe wanaokabiliwa na kero ya migogoro ya ardhi,ndoa pamoja na mirathi.
Akizungumzia ujio wa mawakili hao wa kujitolea mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa alisema mawakili hao wanakuja kufutia ofisi yake kupokea mlalamiko ya migogoro hiyo mara kwa mara hivyo ikamlazimu kuandaa tamasha ambalo litakutanisha mawakili,wananchi pamoja na wajasiliamali katika uwanja wa sabasaba.
‘’Tumeandaa tamasha kuanzia tarehe novemba 15 hadi 17 ambalo tumeita wanasheria wa kujitolea mawakili ambao wanatokea mkoa wa Iringa na Njombe kama 20 ambao watatoa msaada wa bure kabisa wa kisheria kwa wananchi’’alisema Kasongwa.
Aliongeza kuwa’’Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu tumeona wananchi wa wilaya ya Njombe wanasumbuka sana na migogoro ya ardhi,ndoa na miradhi na inapelekea matukio mengine kutokea kutokana na kushindwa kumalia matukio yao au zile kesi’’alisema mkuu wa wilaya.
Mkuu wa wilaya alisema kuwa wananchi wa Njombe wakitumia vizuri fursa hiyo itasadia kuepuka migogoro mingi ambayo ipo kisheria ambayo haitatuliwi kwenye upande wa siasa.
‘’Tamasha hili ambalo tumeliandaa litasindikizwa na vitu vingi kama huduma kutoka taasisi zote kutoka tasisi zote za serikali ziliopo wilaya ya Njombe,kutakua na mifuko ya kijamii,tasisi binafsi pia kutakua na huduma za upimaji afya bure kwa magonjwa yote kwa hiyo wananchi wakaribie ili waweze kuja kuona kitu gani ambacho tumewaandalia’’alisema Kissa.
Pia alisema ‘’Mh Raisi wetu mama Samia Suluhu Hassan katika msisitizo wake anatuelekea sisi wasaidizi wake kutatua kero za wannachi na asingependa anapopita kwenye ziara zake kwa wananchi akute wanakero au kuna vitu ambavyo havijatatuliwa ndo maana tunafanya kila linalowezekana pamoja na kuwafikia kwenye maeneo yao tunafanya ubunifu ili wananchi waweze kutatuliwa wengi kwa wakati mchache ili iweze kuleta tija kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu’’alisema.