NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MABINGWA wa
Jamhuri mwaka 1988 African Sports “Wanakimanumanu” wameanza kuzipigia hesabu
pointi tatu kwenye mchezo wao wa Champion Ship dhidi yao na JKT Tanzania utakaopigwa
kesho kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Jijini Tanga
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Idara
ya Mawasiliano ya timu ya African Sports Said Karsandas (Pichani ) alisema kwamba maandalizi kwa upande
wao yamekamilika kwa asilimia 90 huku wachezaji wakiwa na hari kubwa kuelekea
mchezo huo.
Alisema kwamba pamoja na maandalizi ambayo
wameyafanya lakini wataingia kwenye mchezo huo kupambana kufa na kupona
kutokana na aina ya timu ambayo wanakutana nayo yenye uzoefu katika soka .
“Tunatambua kwamba utakuwa ni mchezo mgumu kutokana
na kwamba wapinzani wetu aina ya rasilimali zote na wana wachezaji asilimia 90
walioshuka nao daraja lakini tunaamini kwamba tutaingia kwa lengo la kwenda
kupambana ili tupate matokeo”Alisema
Alisema kwamba licha ya kwamba matokeo sio mazuri kwa
upande wao kutokana na wameshinda mchezo mmoja, sare mitatu wakiwa na pointi
sita huku wakiwa wamepoteza michezo mwili lakini watapambana hadi kieleweke.
“Mechi hii ni ya kufa na kupona ushindi kwetu ni
muhimu kutokana na kwamba utaturudisha kwenye nia sahihi na malengo
tuliojiwekea kwenye msimu huu kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kila mechi”Alisema
Hata hivyo aliwataka wapenzi, mashabiki kujitokeza
kwa wingi kushuhudia mchezo huo ambao utakuwa wa aina yake huku akieleza hizo
ni mbio za kupokezana vijiti.