Waziri wa Afya wa Kenya Mhe. Mutahi Kagwe akitia saini katika kitabu cha wageni pamoja na ujumbe wake kutoka Jamhuri ya Kenya wakati walipotembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai hivi karibuni
Waziri wa Afya wa Kenya Mhe. Mutahi Kagwe pamoja na ujumbe wake kutoka Jamhuri ya Kenya wakiangalia mradi wa mfano wa Bwawa la JNHPP unaotekelezwa na serikali wakati walitembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai hivi karibuni
Waziri wa Afya wa Kenya Mhe. Mutahi Kagwe akieleza jambo wakati akiangalia mfano wa mradi wa Bwawa la JNHPP wakati yeye pamoja na ujumbe wake kutoka Jamhuri ya Kenya walipotembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai hivi karibuni.
……………………………………….
Na Abubakari W Kafumba, UAE
Waziri wa Afya wa Kenya Mhe. Mutahi Kagwe pamoja na ujumbe wake kutoka Jamhuri ya Kenya walitembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai hivi karibuni.
Ujumbe huo ulipokelewa kwa furaha na ukarimu na Mkurugenzi wa Banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai kutoka TanTrade Bi. Getrude Ng’weshemi pamoja na Taasisi za sekta mbalimbali zinazoshiriki kwenye maonesho hayo zikiwemo TANESCO, TTB, TANAPA, TRC, TIC, TPDC, STAMICO, Tume ya Madini na GST.
Mhe. Mutahi amefurahi kujionea namna ambavyo Tanzania inajitanganza kupitia maonesho haya ya Expo 2020 Dubai.
Aidha, Mhe. Mutahi amejivunia kuona Tanzania kama moja ya nchi za Afrika Mashariki kupata nafasi hii adhimu ya kushiriki kwenye maonesho haya kwa ukamilifu huku ikizipa kipaumbele sekta zote muhimu zinazotangaza upekee wa Tanzania kwa upande rasilimali ilizonazo, miradi mikubwa ya kimakakati na fursa za kibiashara zinazowavutia wawekezaji mbalimbali kwa wingi.
Ameongeza kuwa, “Tanzania na Kenya zitaendelea na ukaribu, umoja na ushirikiano kama majirani na ndugu huku faida mojawapo ya kuwa katika maonesho haya ni fursa nzuri ya kuweza kupata wawekezaji katika sekta mbalimbali kwa kuwa maonesho haya yanauleta ulimwengu pamoja, hivyo ni vema kwa Tanzania na Kenya kwa pamoja kutumia fursa ya kuwepo kwenye maonesho haya ya Expo 2020 Dubai kufikia wawekezaji wengine kupitia Dubai”.