Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Rahima Njaidi akizungumzia na wadau wa utunzaji Shirikishi wa misitu kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo mkoani Morogoro.
……………………………………….
Mwandishi wetu-Morogoro
Imeelezwa kuwa sheria ya misitu GN417 imeendelea kuwa changamoto katika vijiji ambavyo vinashiriki dhana ya usimamizi shirikishi wa misitu (USMJ) nchini Tanzania.
Changamoto hiyo imebainishwa na wadau wa misitu ambao ni wanachama wa mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu nchini Tanzania (MJUMITA) katika kikao cha wadau wa usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii.
Wadau hao wamedai kuwa baadhi ya maeneo ambayo yalikuwa yakifanya USM kwa kutumia dhana ya uhifadhi misitu kupitia biashara endelevu ya mazao ya misitu wameanza kupoteza matumaini kutokana na kukosa wateja na upatikanaji wa fedha kupungua mwaka hadi mwaka.
Sadiki Kondo ambaye ni Katibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji Cha Matuli kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro amesema kuwa mapato ya Kijiji Chao yameshuka ambapo kwa mwaka 2018/2019 Kijiji kiliweza kukusanya shilingi milioni 80 huku 2020/2021 Kijiji Cha Matuli kimeweza kuvuna gunia 740 tu.
“Fedha tulizokuwa tunapata zilitusaidia kufanya Mambo mengi sana mfano Matuli tulichangia kujenga madarasa mawili ya shule ya msingi,kuwapatia wananchi CHF iliyoboreshwa Kijiji kizima,Kujenga matundu 20 ya vyoo shule ya msingi,kuchangua milioni 12 Sekondari na kuchimba visima sita vya maji na kupata fedha ya uhifadhi kwa ajili ya msitu wetu wa Kijiji lakini katika mwaka 2021/2021 tumeshindwa kufanya chochote sababu mapato yameshuka hivyo GN 417 imetuletea changamoto hiyo hivyo wadau na Serikali waitazame upya.”Sadiki Kondo.
Saimon Lugazo ni Afisa uwezesha kutoka Shirika la kuhifadhi misitu ya asili nchini Tanzania ameiomba Serikali kuingalia upya GN 417 kwa kuwa inaweza kuchochea uharibifu wa misitu katika maeneo ambayo wananchi walikuwa wakitunza misitu hiyo.
“Moja ya changamoto ni miongozo iliyotoka ya bei ya ushuru elekezi ya 12500 kwa gunia la mkaa kwa hiyo vijiji vinginambavyo havifikiki uzalishaji na mapato yameshuka sana, tunajua sheria ishapitishwa lakini inaweza ikatazamwa upya kutokana na changamoto ambazo zimejitokeza,sababu wananchi wasipopata kitu Cha kuwashawishi wanaweza kubadilisha matumizi ya misitu na pengine kupelekea uharibifu kurejea Tena.”Saimon Lugazo Afisa uwezeshaji TFCG.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Bi Rahima Njaidi amewashauri wanachi kutoka maeneo mbalimbali ambayo kumekuwa na mkinzano wa sheria ndogo na sheria mama kukaa pamoja na kuzitathimi sheria hizo ili kuondoa mkanganyiko uliopo.
“Tumepokea.malalamiko kutoka maeneo mengi sana ya kukinzana kwa sheria ndogo za vijiji na sheria mama ambayo imekuwa ikirudisha nyuma Ari ya wananchi katika utunzaji wa misitu ya vijiji hivyo wake chini ili kuangalia namna gani wanamakiza mikinzano hiyo” Rahima Njaidi Mkurugenzi MJUMITA.
Warsha hiyo imekusanya wadau kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Morogoro,Kilosa, Mvomero,Tunduru,Lindi, Liwale,Ruangwa na Iringa ambapo wadau wamepata nafasi ya kubadilishana ujuzi na uzoefu katika utunzaji wa misitu.