Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) tawi la Shinyanga imewashukuru na kuwapongeza Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushiriki kikamilifu katika Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon”.
Mbio hizo za hisani za kimataifa ‘NBC Dodoma Marathon’ zilizoandaliwa na Benki ya NBC zimefanyika Novemba 7,2021 jijini Dodoma na kufanikiwa kukusanya fedha zaidi ya Mil 200 kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya Saratani ya mlango wa Kizazi kwa akina mama.
Akizungumza leo Jumatatu Novemba 8,2021 na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi PJFCS katika Bwalo la Polisi Mjini Shinyanga Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Fredrick Rutta amesema Benki ya NBC imefarijika sana kwa uwakilishi mkubwa wa PJFCS katika Mbio za NBC Dodoma Marathon.
“Sisi NBC Kimsingi tumefarijika sana kwa kikundi hiki cha PJFCS kwa uwakilishi mkubwa waliouonesha, hii inaonesha ni kwa jinsi gani kikundi hiki kipo tayari kujitoa kwa jamii kama Benki ya NBC inavyofanya. Naomba tuendeleze ushirikiano huu”,amesema Rutta.
“Tunachukua nafasi kuwashukuru na kuwapongeza sana wanamichezo kutoka PJFCS walioshiriki kwenye Mbio za NBC Marathon na wote walioonekana kwenye orodha ya washindi 10 bora. Wapo waliojitokeza kwenye TOP Ten, hii inaonesha ni kiasi gani Shinyanga tuko vizuri kwenye Riadha. Na sisi benki ya NBC bado tutaendelea kufanya mbio za Marathon”,ameongeza Rutta.
Rutta akiwa ameambatana na maafisa kutoka Benki ya NBC amekabidhi vinywaji baridi zikiwemo soda, juisi na maji kwa ajili ya Wana michezo wa kikundi cha PJFCS.
Rutta ametumia fursa hiyo kuwaomba Wana Michezo wa kikundi cha PJFCS na wananchi kwa ujumla kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya NBC ikiwemo Mikopo kwa Wajasiriamali na Watumishi kwa riba nafuu.
“NBC pia tuna Akaunti maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali (Kua Nasi Account) ambazo hazina makato mwisho wa mwezi na unapata faida ya asilimia 2 kwa mwezi. Hali kadhalika tuna Akaunti za Kiuwekezaji (Malengo Account ambayo tunakupa hadi aslimia saba kulinga kiasi cha pesa ulichonacho kwenye akaounti na Akaunti za muda maalum ambazo nazo riba zake ni shindani sana sokoni ) pamoja akaunti za Vikundi ambazo hazina makato mwisho wa mwezi na tunakupa faida ya asilimia hadi 2 kwa mwaka”,amefafanua Rutta.
Makamu Mwenyekiti wa PJFCS, Lucas Moris ameishukuru Benki ya NBC kwa kuandaa Mbio hizo na kwamba wameshiriki kikamilifu katika mbio hizo na kufanikiwa kuutangaza na kuupa heshima mkoa wa Shinyanga.
“Tulikwenda kushiriki NBC Dodoma Marathon kuwakilisha mkoa wa Shinyanga kama kikundi cha mazoezi, safari yetu imeenda vizuri, tulienda washiriki 25, tumekimbia na wote tumefanikiwa kufikia malengo ambayo tulikuwa tunayataka, wote tumemaliza kilomita zote kadri tulivyokuwa tumejiandikisha, ambapo mashindano yalikuwa na Kilomita 42,21,10 na kilomita 5”,amesema Moris.
Moris ametumia fursa kuwashukuru viongozi wa mkoa wa Shinyanga akiwemo Mkuu wa Mkoa Mhe. Sophia Mjema na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando kwa ushirikiano na msaada wa hali na mali waliouonesha kufanikisha Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) kushikiriki katika mbio hizo za NBC Dodoma Marathon.
Katika mbio hizo zilizofanyika jijini Dodoma na kupambwa na uwepo wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ilishuhudiwa Mwanariadha Mtanzania Tumaini Habie akiiibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za KM 42 upande wa wanaume baada ya kumaliza kwa muda wa saa 02:17:15, akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya Eyanae Paul aliyetumia muda wa saa 02:18:31.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Fredrick Rutta akizungumza na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga na kuwapongeza kwa kushiriki kikamilifu katika Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon”. Kushoto ni Mhasibu wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga Bi. Maristella
Isundwa, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa PJFCS, Lucas Moris.
Isundwa, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa PJFCS, Lucas Moris.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Fredrick Rutta akizungumza na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga na kuwapongeza kwa kushiriki kikamilifu katika Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon”.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Fredrick Rutta akizungumza na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) inayolelewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga na kuwapongeza kwa kushiriki kikamilifu katika Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon”.
Makamu Mwenyekiti wa PJFCS, Lucas Moris akielezea namna walivyoshiriki kikamilifu katika Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon” na kuutangaza mkoa wa Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa PJFCS, Lucas Moris akielezea namna walivyoshiriki kikamilifu katika Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon” na kuutangaza mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa PJFCS, Idrisa Kibira akielezea namna walivyoshiriki kikamilifu katika Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon” na kuutangaza mkoa wa Shinyanga.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga, Fredrick Rutta (kushoto) akimkabidhi maji Mwenyekiti wa PJFCS, Idrisa Kibira kwa ajili ya Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS).
Zoezi la kukabidhi vinywaji bariki kwa ajili ya Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) likiendelea.
Maafisa kutoka Benki ya NBC wakipiga picha ya kumbukumbu na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) walioshiriki Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon”.
Maafisa kutoka Benki ya NBC wakipiga picha ya kumbukumbu na Wana Michezo wa Klabu ya Mazoezi maarufu Polisi Jamii Fitness Center Shinyanga (PJFCS) walioshiriki Mbio za hisani za kimataifa “NBC Dodoma Marathon”.
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog