WENYEJI, Chelsea wamelazimishwa sare ya 1-1 na Burnley katika mchezo wa Ligi ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijiji London.
Kai Havertz alianza kuifungia The Blues dakika ya 33 kabla ya Matej Vydra kuisawazishia Burnley dakika ya 79.
Chelsea inafikisha pointi 21 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Manchester City, wakati Burnley inafikisha pointi nane baada ya wote kucheza mechi 11.