Washiriki wa majadiliano yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya wakisikiliza namna Tanzania inavyoweza kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia pamoja na namna Tanzania itakavyonufaika na Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kukamilika mbali na kuzalisha umeme.
Washiriki wa majadiliano yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya wakisikiliza namna Tanzania inavyoweza kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia pamoja na namna Tanzania itakavyonufaika na Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kukamilika mbali na kuzalisha umeme.
Naibu Muidhinishaji Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Jonathan Mpuya akifungua sehemu ya pili ya majadiliano leo mkoani Dar es Salaam. Mjadala unaendelea umeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya ukiangalia namna Tanzania inavyoweza kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia pamoja na namna Tanzania itakavyonufaika na Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kukamilika mbali na kuzalisha umeme.
……………………………………..
Na Mwandishi Wetu
WADAU mbalimbali wanaoshiriki kwenye kongamano kuhusu sera za namna Tanzania inavyoweza kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia linalofanyika mkoani Dar es Salaam, wametoa mapendekezo mbalimbali kwa serikali ikiwemo kusimamia vyema maofisa ugani ili kuongeza uzalishaji.
Kongamano hilo lilifunguliwa na Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda jana, akisema Tanzania inazalisha asilimia 45 tu ya mafuta ya kupikia na hivyo kulazimika kuagiza nje kiasi kilichobaki ili kutoshekeza mahitaji na kutumia Sh bilioni 475 ambazo alisema zingetumika kuboresha uchumi wa ndani.
Katika mijadala yao, Wadau hao kutoka sekta mbalimbali wanasema kuna maofisa ugani ambao wanasubiri tu mshahara lakini hawatekelezi majumu yao ipasavyo na hivyo wakashauri ikiwezekana serikali ianze kufikiria kuwa na maofisa ugani wanaotoka sekta binafsi kwani kuna nchi zinafanya hivyo na kupata mafanikii.
Akisoma maoni ya kundi namba moja la mjadala katika kongamano hilo, Frank Reuben ambaye anatoka Tasisi ya Utafiti wa Kilimo (Tari), alisema wanaishauri serikali kuanzisha mashamba darasa mengi ya mazao yanayozalisha mafuta ya kupikia kutokana na umuhimu wake.
Tanzania inahamasisha kilimo cha alizeti kama mkakati wa muda mfupi wa kupambana na uhaba wa mafuta huku mkakati wa muda mrefu ukiwa ni uzalishaji wa chikichi. Mazao mengine yanayotoa mafuta ni pamba, ufuta, karanga na nazi.
Kwa upande wa utafiti washiriki hao wa kongamano kupitia kundi namba mbili waliitaka serikali iweke muunganiko mzuri baina ya watafiti na wananchi wakishauri ikiwezekana wananchi washirikishwe kwenye tafiti lakini kubwa wakitaka matokeo ya tafiti yawaikie wananchi.
Walisema pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya kimkakati na yaliyozoeleka washiriki wa kognamano pia waliitaka serikali kutafiti mazao mengine yanayotoa mafuta yakiwemo ambayo hayalimwi nchini kama makademia.
Kongamano hilo linaendelea leo kwa kuangalia faida zitakazopatikana baada ya kuanza kuzalishwa kwa umeme wa maji wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP).
Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.
Linashirikisha maofisa wa serikali, taasisi binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi zinazojihusisha mada husika na waandishi wa habari.