Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Joseph Mkirikiti, akizungumza wakati wa mafunzo kwa wadau wa sekta ya usafirishaji yaliyoandaliwa na TANROADS, leo Oktoba 3, 2021, Mkoani Rukwa
Amesema “Kuna watu tunawajua wana malori mengi barabarani wakiwemo wakina Bakhresa na Asas, lakini hawa ndiyo watekelezaji wakubwa wa sheria ipasavyo, nitoa rai kwa TANROADS kuwatengenezea hata nishani watu wa namna hii”.
“Tunapopeana hizi elimu tutambuane pia wale wanaozingatia sheria na kama inafaa basi tuwape tuzo na hivyo hivyo hata kwa ngazi ya watendaji wetu wa mizani, nao lazima tujue nani anafanya kwa mujibu wa sheria”.
“Kutuchagua sisi kuwa wenyeji wa mafunzo haya ni jambo la fahari sana, kwa sababu Mkoa huu unafunguka kwa pande zote, tunalojadili hapa ni suala la maendeleo. Iwapo Mkoa huu utatumika vizuri utakuwa lango la bidhaa zinazotoka Congo”.
“Kujipanga kimkakati katika utunzaji wa miundombinu ya barabara, kunalenga kupandisha pato la Mkoa wetu na taifa, kwa kiwango kikubwa ni miundombinu iliyotunzwa vizuri ndio inatusaidia kusafirisha bidhaa kupeleka sokoni na kukuza pato”.