**********************************
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amewataka wasanii kote nchini kuwa na nidhamu ya hali ya juu ili kupata mafanikio kufika katika ngazi za Kimataifa.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2021 kwenye Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni wakati alipokuwa live kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm Radio kilichofanyikia kwenye eneo la Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Amesema wasanii wanatakiwa kudumisha maadili ya kitanzania ili kuendelea kuitangaza nchi yetu badala ya kuiga tabia mbalimbali za wasanii wa nje ambazo hazina maadili katika Taifa letu.
Mkuu wa Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo Dkt. Herbet Makoye amesama chuo kinaendelea kutoa elimu mbalimbali za sanaa ambapo amewataka kujiongeza baada ya kumaliza masomo yao.
Dkt. Makoye amewataka wadau mbalimbali kufika kwenye Tamasha la Bagamoyo ili kubadilishana uzoefu.
Tamasha hilo ni la siku tatu kuanzia Oktoba 28-30, 2021 ambapo lengo kuu la Tamasha hilo ni kuboresha Sanaa na Utamaduni wetu.