Baadhi ya Wanafunzi kutoka Chuo Cha Microtech kilichopo Mpendae Mjini Zanzibar, Wakiskiliza mafunzo ya Udhalilishaji wa Kingono yaliyotolewa na Mkufunzi kutoka Jumuiya ya wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Amriya Ahmedi Moh’d (hayupo pichani).

Mkufunzi kutoka Jumuiya ya wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Amriya Ahmedi Moh’d akitoa mafunzo ya Udhalilishaji wa Kingono kwa Wanafunzi wa Chuo cha Microtech huko  Mpendae Mjini Zanzibar .

Mwalimu kutoka chuo cha Microtech kilichopo Mpendae Mjini Zanzibar, Saadam Mkopi Ali akiwaeleza Wanafunzi wa chuo hicho juu ya umuhimu wa elimu ya udhalilishaji wa kingono.

Mkufunzi kutoka Jumuiya ya wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Amriya Ahmedi Moh’d akionyesha picha inayoashiria kupinga udhalilishaji wa kingono , wakati akitoa Mafunzo  kwa Wanafunzi wa Chuo cha Microtech huko  Mpendae Mjini Zanzibar .

Mwanafunzi kutoka Chuo cha Microtech kilioko Mpendae Mjini Zanzibar , Amour Mwinyi Ali akielezea jinsi anavofahamu udhalilishaji wa kingono.

Picha Na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar.