Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akimkabidhi zawadi ya picha ya mlima Kilimanjaro kiongozi mkuu wa kanisa la Greek Orthodox Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam.
Kiongozi mkuu wa kanisa la Greek Orthodox Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa) akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na kiongozi mkuu wa kanisa la Greek Orthodox Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa) Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na kiongozi mkuu wa kanisa la Greek Orthodox Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa) Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na kiongozi mkuu wa kanisa la Greek Orthodox Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa) Ikulu jijini Dar es salaam.
…………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Oktoba 24,2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa)Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Greek Orthodox Ikulu Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais amesema Tanzania imefurahishwa na ujio wa Baba Mtakatifu huyo na kumuomba kuendelea kuiweka nchi ya Tanzania katika maombi yake ya kila siku. Amesema tangu kupata uhuru Tanzania imekua kitovu cha Amani na kuendelea kuheshimu umuhimu wa dini zote kupitia ibara ya 19 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha amesema viongozi wa dini nchini Tanzania wamekua ndio msingi wa Amani iliopo nchini.
Makamu wa Rais ameongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za dini hapa nchini kwa kushirikiana vema na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo husasani katika sekta za elimu na afya hasa katika maeneo ya pembezoni ya nchi. Ametaja mchango wa kanisa la Orthodox nchini ambao ni pamoja na ujenzi Kliniki 90 pamoja na Hospitali katika mkoa wa kagera na shule katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Amesema Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na kanisa la Orthodox hapa nchini pamoja na dini zingine katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa) Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Greek Orthodox amesema amefurahishwa kushiriki mazungumzo na Makamu wa Rais na kumuomba kufikisha salamu zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amemtaja kama mfano wa upendo unaopatikana nchini Tanzania. Amesema Tanzania ni nchi imara sana ambayo amekua akiitaja katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo alipofanya ziara nchini Russia na kukutana na Rais wa nchi hiyo Vladmir Puttin alipoulizwa juu nchi imara barani Afrika aliitaja Misri ikifuatiwa na Tanzania.
Amesema uimara wa Tanzania unatambulishwa na uwepo wa watu imara pamoja na fursa nyingi zilizopo huku ikijitambulisha vema duniani kwa mazuri yake. Aidha ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Hayati John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania na kuahidi kuwa ataendelea kuiombea mema Tanzania na watu wake wakati wote atakapokuwa Alexandria Nchini Misri.
Aidha Baba mtakatifu huyo amesema Tanzania imezidi kuongeza idadi ya waumini wa kanisa la Orthodox na tayari wameanza ujenzi wa kituo kikubwa cha maombezi jijini Arusha ambacho kitakua ndio kitovu cha maombi katika nchi za Afrika Mashariki.