Home Siasa TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI JIMBO LA NGORONGORO

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI JIMBO LA NGORONGORO

0
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha ,Juma Mhina akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi Jimbo la Ngorongoro (Happy Lazaro)
………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngorongoro Juma Mhina amesema kuwa,Tume ya uchaguzi ya Taifa imetangaza uchaguzi rasmi katika Jimbo la Ngorongoro  na  tayari amepokea barua rasmi ya kusimamia ,hivyo  ameomba upendo,amani na mshikamano  pamoja na ushirikiano kwani nchi nzima mahali penye uchaguzi  pekee ni Jimbo la Ngorongoro tu .
Amesema kuwa,idadi ya Wapiga kura kwa mujibu daftari la Wapiga kura la mwaka   2020   ni wapigakura 11,500 wa jimbo hilo la Ngorongoro  na vituo vya  kupiga kura vikiwa ni 310. 
Amesema kuwa, Tume inavielekeza vyama vya siasa vyote waanze mchakato wa kutafuta wagombea katika vyama vyao  vyao vya siasa  kuanzia tarehe  18 hadi 24 mwezi wa kumi.
Mhina amesema kuwa,tume itaanza mchakato wa kutoa fomu kwa wagombea mbalimbali  kuanzia  tarehe 7 hadi  15/mwezi wa 11.
Ameongeza kuwa,kuanzia tarehe 15/11/2021 Tume itaanza kazi ya uteuzi kwa wagombea kutoka vyama mbalimbali ambao watakidhi vigezo vya kugombea .
Mhina  amefafanua kuwa ,kuanzia tarehe 16 /11 hadi tarehe 10/12 itakuwa siku ya kampeni  ambapo  wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa wataanza kufanya Kampeni za kujinadi.
Amesema kuwa,tarehe 11/12 / 2021 itakuwa siku ya kupiga kura ya kumtafuta mgombea atakayeshinda kupeperusha bendera ya jimbo hilo .
Uchaguzi huo umerudiwa baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, William Ole Nasha kufariki dunia 22/9/2011.