Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha ,Juma Mhina akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi Jimbo la Ngorongoro (Happy Lazaro)
………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngorongoro Juma Mhina amesema kuwa,Tume ya uchaguzi ya Taifa imetangaza uchaguzi rasmi katika Jimbo la Ngorongoro na tayari amepokea barua rasmi ya kusimamia ,hivyo ameomba upendo,amani na mshikamano pamoja na ushirikiano kwani nchi nzima mahali penye uchaguzi pekee ni Jimbo la Ngorongoro tu .
Amesema kuwa,idadi ya Wapiga kura kwa mujibu daftari la Wapiga kura la mwaka 2020 ni wapigakura 11,500 wa jimbo hilo la Ngorongoro na vituo vya kupiga kura vikiwa ni 310.
Amesema kuwa, Tume inavielekeza vyama vya siasa vyote waanze mchakato wa kutafuta wagombea katika vyama vyao vyao vya siasa kuanzia tarehe 18 hadi 24 mwezi wa kumi.
Mhina amesema kuwa,tume itaanza mchakato wa kutoa fomu kwa wagombea mbalimbali kuanzia tarehe 7 hadi 15/mwezi wa 11.
Ameongeza kuwa,kuanzia tarehe 15/11/2021 Tume itaanza kazi ya uteuzi kwa wagombea kutoka vyama mbalimbali ambao watakidhi vigezo vya kugombea .
Mhina amefafanua kuwa ,kuanzia tarehe 16 /11 hadi tarehe 10/12 itakuwa siku ya kampeni ambapo wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa wataanza kufanya Kampeni za kujinadi.
Amesema kuwa,tarehe 11/12 / 2021 itakuwa siku ya kupiga kura ya kumtafuta mgombea atakayeshinda kupeperusha bendera ya jimbo hilo .
Uchaguzi huo umerudiwa baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, William Ole Nasha kufariki dunia 22/9/2011.