Murugenzi wa Kampuni ya Chief Promotions Dr. Amon Mkoga akipokea medali na fulana kutoka kwa Di Yun Mkurugenzi wa Kampuni ya King Lion ambao ni wadhamini kwa ajili ya washiriki wa mbio za Mazingira Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 14 kwenye viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es Salaam
Murugenzi wa Kampuni ya Chief Promotions Dr. Amon Mkoga akiponesha namba ya kujisajili kwa ajili ya kushiriki mbio za Mazingira Marathon kushoto ni Di Yun Mkurugenzi wa Kampuni ya King Lion ambao ni wadhamini wa mbio hizo. zinazotarajiwa kufanyika Novemba 14 kwenye viwanja vya Farasi Oysterbay jijini Dar es Salaam
Murugenzi wa Kampuni ya Chief Promotions Dr. Amon Mkoga akipokea akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katikati ni Di Yun Mkurugenzi wa Kampuni ya King Lion na kulia ni Erasto Baragamba meneja Rasilimali watu King Lion.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Inspector Haroun akizungumza katika mkutano huo uliofanyika leo.
……………………………………………..
Murugenzi wa Kampuni ya Chief Promotions Dr. Amon Mkoga amesema kampuni hiyo imeandaa Mbio kwa mara ya kwanza ziitwazo Mazingira Marathon ambazo zitafanyika katika uwanja wa Green grounds Oysterbay Dar es Salaam maarufu Uwanja wa Farasi Jumapili 14.11.2021
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Golden Tulip Posta jijini Dar es Salaam leo amesema Mgeni Rasmi katika mbio hizo atakuwa Makamu wa Rais Dr.Phillip Mpango,Dhumuni la mbio hizi ni katika kumuunga mkono juhudi za Mhe Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kutunza mazingira na Uzazi salama.
Kauli Mbiu ya mbio hizi ni :Mazingira salama ya uzazi kwa Mama:Kukosa huduma za msingi za afya ya uzazi kunaweza kukasababisha kuongezeka kwa idadi ya vifo vya kina mama na Watoto wakati wa kujifungua hivyo hatua hii ni ya kuokoa maisha.
“Chief Promotions itagawa vifaa vya kusaidia wakati wa kujifungua kwa kina mama na kwenye vituo vya afya Unguja Kusini,Tanga,Tabora na Dar es Salaam ili kuhakikisha usafi na mazingira salama wakati wa kujifungua.
Hatua hizo ni za kuokoa maisha kwa wote mama na mtoto.”Gharama za kujisajili ili kushiriki mbio hizo ni kama ifuatavyo.
KM 21 Kusajili ni shlingi za kitanzania 30,000, 10 KM na KM 5 ni shilingi za kitanzania 25,000 na Usajili kwa ajili ya makundi au vikundi vya Jogging na kadharika itakuwa shinilini za kitanzania 20,000 Ambapo washiriki wote watapata T,shirts,Medali na Bibs namba za kukimbilia.
Mbio hizi zimedhaminiwa na kampuni za Kinglion wauzaji wa Pikipiki,Mabati,wino,Guta , Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries, METL, kupitia MO Extra,Afya water,Securities Printers,TBL,Grano Coffee,Turkish restaurant,Golden Tulip Hotel.
Ukitaka kujisajili au kufahamu mambo mbalimbali kuhusu Taasisi hii tembelea Tovuti zake: www.chiefpromotions.or.tz au www.mazingiramarathon.or.tz.