Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe Basilla Mwanukuzi ametoa mifuko 100 ya saruji kwa kijiji cha Makayo , Tarafa ya Mombo, Wilaya ya Korogwe ili kuunga mkono nguvu za wananchi katika ahadi ya ujenzi wa Zahanati ya kwanza katika kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ametoa msaada huo mkubwa katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa baada ya jamii hiyo ya kabila la wamasai kumualika kama mgeni rasmi katika hafla ya kimila ya kusimikwa vuongozi wa kimika ‘malwaiganani’ miezi 2 iliyopita.
Walimlilia changamoto hiyo ya ukosefu wa Zahanati .
Sambaba na msaada huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe Basilla alishiriki rasmi kuzindua kuchimba msingi wa zahanati hiyo na wananchi kwa ramani ya Halmashauri na kuwaahidi kama ilivyotaratibu Halmashauri itakwenda kumalizia ujenzi huo wa Zahanati ili ukamiliike na huduma ianze kutolewa kwa wananchi katika kijiji cha makayo.
Wananchi walifurahia sana na kushiriki zoezi hilo kwa matumaini makubwa kwa viongozi imara walioteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kama Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mh Basilla Mwanukuzi