Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe Akizungumza na washiriki wa Mkutano wa pili wa Kitaifa unao hamasisha kilimo asilia(Ecological Organic Agriculture) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili.
……………………………….
Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Bashe ameahadi kuwa, Wizara ya Kilimo itaendeleza juhudi zake za kumlinda mkulima na mlaji, na kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kilimo asilia kinafanikiwa(organic agriculture) “Tutahakikisha tunaanzisha kitengo kitakacho shughulikia ‘organic agriculture’ na tutakitengea bajeti kwenye bajeti ya 2021/2022” alisisitiza wakati wa kufungua mkutano huo.
Mkutano huo unahudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Balozi wa Ufaransa, Balozi wa Ubelgiji, na wadau wa maendeleo kutoka nchi mbalimbali.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akiangalia nafaka zilizohifadhiwa kwa kutumia dawa asilia bila kutumia kemikali katika banda la Iles De Paix wakati wa Mkutano wa pili wa Kitaifa unao hamasisha kilimo asilia(Ecological Organic Agriculture) unaofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili.