Mkurugenzi Mtendaji qa TASAF Ladislaus Mwamange akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa TASAF jijini Dar es salaam wakati alipowaelezea namna fedha za UVIKO-19 zilizotolewa na serikali zitakavyotumika kwa wanufaika wa mpango huo.
Picha zikionesha baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji qa TASAF Ladislaus Mwamanga wakatialipokuwa akizungumza nao leo kwenye ukumbi wa TASAF Posta jijini Dar es Salaam.
Imeelezwa kuwa kiasi cha fedha Sh.Bil 5.5 zilizotengwa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF zitaelekezwa katika utoaji wa Ruzuku na utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa kaya za walengwa ili kupata kipato kitakachoziwezesha kaya Hizo kujikwamua kiuchumi na kupunguza athari za UVIKO 19.
Hayo yameelezwa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji qa TASAF Ladislaus Mwamanga wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa taarifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa mpango wa kunusuru Kaya za walengwa wa TASAF.
Mkurugenzi huyo amesema kupitia fedha Hizo kaya za walengwa 40,740 wenye uwezo wa kufanya kazi ambao wanaoishi katika maeneo ya Mijini,watafanyakazi katika miradi ya Jamii na Kulipwa ujira wa wastani wa Sh.135,000 kwa kila kaya ili kufufua na kuimarisha shughuli zao.
“TASAF itazitumia fedha Hizo kuondoa athari za kiuchumi zilizochochewa na mlipuko wa UVIKO -19 kwa kaya za walengwa wa TASAF ambao serikali imedhamiria kuwaondoa katika umaskini wa kipato kwa kuwapatia Ruzuku za kujikimu,ajira
Aidha Mwamange amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali katika kupunguza umaskini wa watanzania wanaoishi kwenye mazingira duni na inafanta jitihada kubwa kupata fedha kutoka vyanzo vya ndani.
“Utoaji wa sehemu ya Mkopo huu nafuu kwa ajili ya mpango wa TASAF ni kielelezo tosha kwamba serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan inawajali wananchi wake hasa wale wanaoishi katika mazingira duni”amesema Mwamange
Vilevile Mwamange amesema Menejimenti ya TASAF kwa mwongozo wa Kamati ya Uongozi ya Taifa itahakikisha maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa walengwa katika maeneo yatakayoanishwa unaanza mara tu baada ya fedha Hizo kupokelewa.