Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. David Kafulila akizungumza na vijana wa UVCCM mkoa wa Simiyu wakati wa maadhimisho ya miaka 20 Bila baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere.
Vijana wa UVCCM wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw.David Kafulila wakati alipozungumza nao katika maadhimisho hayo.
Vijana wa UVCCM wakishangikia wakati Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. David Kafulila alipokiwa akiwahutubia katika maadhimisho hayo.
…………………………………………
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. David Kafulila amesema ,pamoja na Uimara na umadhubuti wa Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kuondokewa na Rais Hayati John Pombe Magufuli , ni kielelezo cha misingi imara ya Taifa iliyoasisiwa na Baba wa taiga Mwl. Nyerere.
,
Ameyasema hayo wakati akizungumza na vijana wa UVCCM mkoa wa Simiyi katika maadhimisho ya miaka 20 bila Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa misingi aliyoiweka ambayo imeweza kulivusha Taifa letu katika majaribu na mitikisiko yote iliyopata kulikabili Taifa tangu uhuru!
Amesema kuwa Mwl. Nyerere alisisitiza mipango na mikakati ya Serikali kujielekeza kwenye mahitaji ya watu ( People Centred Development), Ndicho tunakiona kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
“Hata kwenye mpango wa matumizi ya 1.3 trilion za IMF, kwamba zimeelekezwa kuleta magari 25 ya kuchimba visima, mitambo 5 kuchimba mabwawa, yote kwajili ya kutatua tatizo la maji. Vyuo 32 vya VETA ambapo Simiyu tunaenda kupata chuo 1, madarasa 15,000 ambayo yote ni mambo yanayotibu shida za watu moja kwa moja,”. Amesema David Kafulila.
Ameongeza kuwa pamoja na changamoto zote, Tanzania imepiga hatua kwenye kupunguza umasikini wa huduma.leo kuna huduma ya upasuaji kwenye tarafa wakati zamani ilipaswa kusafiri na kutumia fedha nyingi kuitafuta huduma kuliko gharama ya huduma yenyewe.kuna wakati mtu alitumia 80% ya gharama kutafuta huduma na huduma yenyewe ikawa asilimia 20% tu ya fedha zote alizotumia kufanikisha matibabu.
Aidha amebainisha kuwa upatikanaji maji Simiyu ni asilimia 64% tu. Nikweli kuna tatizo. Lakini muhimu wananchi wanaona na wanajua kuwa kila wilaya kuna miradi ya maji inaendelea kujengwa na zaidi uamuzi wa Mhe.Rais kuleta mitambo 5 ya kuchimba mabwawa, gari 1 la kuchimba visima mkoani Simiyu na mradi wa bomba kutoka ziwa Victoria ni kielelezo kuwa lengo la ilani la kuhakikisha zaidi ya asilimia 85% wanapata maji vijijini ifikapo 2025 ni bayana na hakika linakwenda kutekelezwa kikamilifu.
Kafulila amefafanua kuwa umasikini wa kipato kwa tafsiri ya benki ya dunia ni mtu kupata chini ya dola 2 kwa siku au chini ya 6600/=. Nikweli bado kuna tatizo lakini kuna nafuu kubwa ukilinganisha na wenzetu kwani wakati asilimia 26% ya watu watanzania ni masikini kwa tafsiri hiyo, Kenya ni asilimia 36% , Rwanda 38% , Zambia 54% na Afrika kusini 55% kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya dunia.
Amemalizia kwa kusema watumiaji wadogo wa umeme vijijini kutozwa Tsh.100/= wakati wastani wa bei ya umeme ni Tsh.230/= kwa unit ni misingi ya fikra za Mwl. Nyerere kupunguza tofauti ya aliyenacho na asiyenacho.