WENYEJI, Watford FC wametandikwa mabao 5-0 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vicarage Road, Watford.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na washambuliaji Msenegal, Sadio Mané dakika ya tisa, Mbrazil Roberto Firmino dakika ya 37, 52 na 90 na Mmisri Mohamed Salah dakika ya 54.
Liverpool wanafikisha pointi 18 baada ya ushindi huo kwenye mchezo wa nane.
Kwa ushindi huo kwenye mchezo ambao kipa Msenegal, mzaliwa wa Ufaransa, Edouard Mendy alijizolea sifa kemkem kwa kuokoa michomo mingi, Chelsea inafikisha pointi 19 na kurejea kileleni sasa ikiizidi pointi moja Liverpool baada ya wote kucheza mechi nane.