Home Michezo MAN CITY YANG’ARA NYUMBANI,MAN UNITED YACHAPWA 4-2 NA LEICESTER CITY

MAN CITY YANG’ARA NYUMBANI,MAN UNITED YACHAPWA 4-2 NA LEICESTER CITY

0

MABAO ya Bernardo Silva dakika ya 12 na Kevin De Bruyne dakika ya 70 yameipa Manchester City ushindi wa 2-0 dhidi ya Burnley:l leo Uwanja wa Etihad Jijiji Manchester.
Kwa ushindi huo, kikosi cha kocha Mspaniola, Pep Guardiola kinafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja tu na Liverpool baada ya wote kucheza mechi nane.

WENYEJI, Leicester City wamewatandika Manchester United mabao 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa King Power, Leicester, Leicestershire.
Mabao ya Leicester City yamefungwa na Youri Tielemans dakika ya 31, Caglar Soyuncu dakika ya 78, Jamie Vardy dakika ya 83 na mshambuliaji Mzambia, Patson Daka dakika ya 90, wakati ya Man United yamefungwa na Mason Greenwood dakika ya 19 na Marcus Rashford dakika ya 82.